Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ

Maswali na Majibu kuhusu Hukumu ya Mwisho

โ€ข
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Ufufuko wa wafu maana yake nini?
Ufufuko wa wafu maana yake mwisho wa dunia watu wote watafufuka na miili yao na kwenda nayo katika furaha ya milele au moto wa milele. (Ayu 19:25-26, Mt 22:30-32, Yh 28-29)

Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?
Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi.

Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?
Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46)

Mbinguni ni mahali pa namna gani?
Mbinguni ni makao mema ya heri na furaha (2Kor 5:1, Ufu, 2:17).
Waendao mbinguni ni wale wanaokufa katika hali ya neema ya utakaso na urafiki na Mungu na waliotakaswa kikamilifu

Motoni ni nini?
Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15)

Uzima wa milele ni nini?
Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho.

Toharani ni mahali gani?
Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).

Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?
Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)

Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?
Mambo hayo ni;
1. Kifo
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)

Je, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia?
Ndiyo, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa.
Mwenyewe alisema, โ€œMimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata mileleโ€ (Yoh 11:25- 26).
โ€œKristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtuโ€ (1Kor 15:20-21).
โ€œAlitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa hakiโ€ (Rom 4:25).

Je, ni muhimu tujiandae kufa?
Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa โ€œkufa mara moja, na baada ya kufa hukumuโ€ (Eb 9:27).
โ€œKatika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatimaโ€ (YbS 7:36).
โ€œHamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutowekaโ€ (Yak 4:14).
โ€œKesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuniโ€ (Math 26:41).

Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?
Ndiyo, โ€œina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wakeโ€ (Zab 116:15).
Hasa utiifu wa Yesu msalabani umegeuza laana ya kifo iwe baraka kwa waamini wake.
โ€œHeri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana naoโ€ (Ufu 14:13).

Tutakapofariki dunia itatutokea nini?
Tutakapofariki dunia roho yetu isiyokufa, mbali na mwili unaooza, itapewa tuzo au adhabu tuliyostahili kwa maisha yetu. โ€œIkawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwakeโ€ (Lk 16:22-23). โ€œKwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faidaโ€ฆ ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sanaโ€ (Fil 1:21,23). โ€œNasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwanaโ€ (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni โ€œmavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoaโ€ (Mhu 12:7). Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele. โ€œPumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mnoโ€ (Ez 37:10).
Je baada ya kufa ni hapo hapo roho inaenda motoni au mbinguni, Au ni mpaka Siku ya hukumu Yesu Atakaporudi?
Ni siku ile ile Roho ya mtu aliyekufa inaenda Mbinguni, toharani au Motoni. Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
"Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako." 43 Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi." (Luka 23:42-43)
Sauli aliweza kuongea na Samweli hata baada ya kufa na Samweli alimbashiria mambo yatakayotokea kwa Sauli maanake ni kwamba Japokuwa alikuwa amekufa bado anayomuungano na Mungu ndio maana aliweza kumwambia Sauli mambo yatakayompata,
"7Basi Sauli akawaambia watumishi wake, โ€œNitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ili nimwendee nipate kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, โ€œYuko mwanamke mmoja huko Endori.โ€ 8Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, โ€œNibashirie na unipandishie huyo nitakayekutajia,โ€ 9Huyo mwanamke akamwambia, โ€œWewe unajua lile alilofanya mfalme Sauli. Amewakatilia mbali wapunga pepo, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?โ€ 10Sauli akamwapia huyo mwananmke kwa Jina la BWANA, akasema, โ€œKwa hakika kama BWANA aishivyo, hutaadhibiwa kwa ajili ya jambo hili.โ€ 11Ndipo yule mwanamke akauliza, โ€œJe unataka nikupandishie nani? Sauli akasema, โ€œNipandishie Samweli.โ€ 12Yule mwanamke alipomwona Samweli alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamwuliza Sauli, โ€œMbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.โ€ 13Mfalme akamwambia, โ€œUsiogope. Unaona nini? Yule mwanamke akasema, โ€œNaona Mungu anapanda kutoka ardhini.โ€ 14Sauli akamwuliza, โ€œNi mfano wa nini?โ€ Yule mwanamke akasema, โ€œNi mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.โ€ Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi uso wake hadi ardhini. 15Samweli akamwuliza Sauli, Kwa nini unanitaabisha, kunipandisha juu?โ€ Sauli akasema, โ€œMimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe lakufanya.โ€ 16Samweli akamwuliza, โ€œKwa nini uniulize mimi, maadam BWANA amekuacha na kuwa adui yako? 17BWANA ametenda lile alilotangulia kusema kwa kupitia kwangu. BWANA ameurarua ufalme kutoka mikononi mwako, naye amempa mmoja wa jirani zako, yaani, Daudi. 18Kwa sababu wewe hukumtii BWANA, wala hukumtimizia ghadhabu yake kali juu ya Waamaleki, BWANA amekutendea mambo haya leo. 19Zaidi ya hayo, BWANA atawatia Israeli pamoja na wewe mkononi mwa Wafilisti na kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia atalitia jeshi la Israeli mkononi mwa Wafilisti.
Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro Yesu alisimulia hivi
19 Akasema, โ€œPalikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake. 22 โ€œHatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, โ€˜Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.โ€™ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, โ€˜Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.โ€™ 27 Akasema, โ€˜Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.โ€™ 29 Ibrahimu akamjibu, โ€˜Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.โ€™ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 โ€˜Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.โ€™ 31 โ€œIbrahimu akamwambia, โ€˜Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.โ€โ€™ (Luka 16:19-31)
Wakati Yesu anabadilika Sura walitokea Musa na Eliya.
"Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. 2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. 4 Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya." (Mathayo 17:1-5)
Yesu alituambia kuwa Mungu sio wa wafu bali wa walio hai ndio maana akaitwa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kuwa Wote wako hai kwake.
37Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila keteketea, alipomwita Bwana โ€˜Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki na Mungu wa Yakobo.โ€™ 38Yeye Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai, kwa kuwa Kwake wote ni hai.โ€ (Luka 20:37-38)
Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
"Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako." 43 Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi." (Luka 23:42-43)
Angalia pia wakati Stefano akipigwa Mawe aliikabidhi roho yake kwa Mungu baada ya kuona mbingu zimefunguka hii ni kama Yesu alivyokuwa pale msalabani aliikabidhi Roho yake kwa Baba yake.
55Lakini yeye Stefano akiwa amejazwa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 56Akasema, โ€œTazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.โ€™โ€™ 57Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 58Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni mwa kijana mmoja aitwae Sauli. 59Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, โ€œBwana Yesu, pokea roho yanguโ€ 60Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, โ€œBwana usiwahesabie dhambi hii.โ€™โ€™ Baada ya kusema haya, akalala. (Mdo 7:55-60)
Kwenye Ufunuo tunasoma (Ufunuo 6:9-10) โ€œNa alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.โ€
Kwa hiyo mtu akifa anaenda mbinguni au motoni kulingana na alivyoishi.
โ€œNasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwanaโ€ (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni โ€œmavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoaโ€ (Mhu 12:7).
Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele.
โ€œKwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faidaโ€ฆ ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sanaโ€ (Fil 1:21,23).
Mtume Petro ameandika hiviโ€ฆ
"18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji." (1Petro 3:18-20)

Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?
Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake.
โ€œNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtumaโ€ (Yoh 17:3).
โ€œKwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaaโ€ (2Pet 1:3-4).
Sisi tuliobatizwa tunaitwa โ€œwana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!โ€ (1Yoh. 3:1).
Kwa sababu tumesadiki kwamba โ€œMungu ni upendoโ€ (1Yoh 4:8) na kwamba โ€œhakuna lisilowezekana kwa Bwanaโ€ (Lk 1:37).
โ€œNa kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Munguโ€ (Gal 4:6-7).

Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?
Aliyezungumzia moto wa milele ni hasa Yesu: akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee, alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo:
โ€œOndokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zakeโ€ (Math 25:41).
โ€œHumo funza wao hafi, wala moto hauzimikiโ€ (Mk 9:48).
โ€œNa moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usikuโ€ (Ufu 14:11).

Toharani maana yake nini?
Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo โ€œalichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zaoโ€ (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: โ€œKama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?โ€ (1Kor 15:29).

Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?
Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > โ€œhupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibikaโ€ (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo โ€œndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingiโ€ (Lk 21:27).
โ€œSaa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumuโ€ (Yoh 5:28-29).
โ€œNa hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa mileleโ€ (Math 25:46).

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?
Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la.
โ€œImetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyopenda, kwamba ni mema au mabayaโ€ (2Kor 5:10).
โ€œBasi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Munguโ€ (1Kor 4:5).
โ€œHapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, โ€˜Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijiaโ€ฆ Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimiโ€™โ€ (Math 25:31-36,40).
โ€œHeri wenye rehema, maana hao watapata rehemaโ€ (Math 5:7).

Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?
Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa.
โ€œKama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yakeโ€ (2Pet 3:13).
โ€œNa Roho na Bibi arusi wasema, โ€˜Njoo!โ€™ naye asikiaye na aseme, โ€˜Njoo!โ€™โ€ฆ Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, โ€˜Naam, naja upesiโ€™. Amina. Na uje, Bwana Yesu! Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Aminaโ€ (Ufu 22:17,20-21).


AckySHINE Solutions
โœจ Join AckySHINE for more features! โœจ

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
๐Ÿ‘ฅ Elijah Mutua Guest Jun 26, 2024
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
๐Ÿ‘ฅ Mary Kidata Guest Jan 16, 2024
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
๐Ÿ‘ฅ Joy Wacera Guest Dec 25, 2023
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
๐Ÿ‘ฅ Anna Sumari Guest Dec 13, 2023
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
๐Ÿ‘ฅ John Mwangi Guest Nov 25, 2023
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
๐Ÿ‘ฅ Kevin Maina Guest Aug 22, 2023
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
๐Ÿ‘ฅ Charles Mrope Guest Feb 23, 2023
Katika imani, yote yanawezekana
๐Ÿ‘ฅ Edith Cherotich Guest Dec 26, 2022
Rehema hushinda hukumu
๐Ÿ‘ฅ Samuel Omondi Guest Dec 21, 2022
Neema ya Mungu inatosha kwako
๐Ÿ‘ฅ Carol Nyakio Guest Dec 1, 2022
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
๐Ÿ‘ฅ Peter Tibaijuka Guest Jun 12, 2022
Mwamini Bwana; anajua njia
๐Ÿ‘ฅ Ruth Mtangi Guest Feb 21, 2022
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
๐Ÿ‘ฅ Lydia Wanyama Guest Dec 26, 2021
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
๐Ÿ‘ฅ Charles Wafula Guest Dec 20, 2021
Nakuombea ๐Ÿ™
๐Ÿ‘ฅ Alice Jebet Guest Oct 11, 2021
Mungu ni mwema, wakati wote!
๐Ÿ‘ฅ Nancy Akumu Guest Jun 5, 2021
Sifa kwa Bwana!
๐Ÿ‘ฅ Stephen Kikwete Guest Mar 6, 2021
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
๐Ÿ‘ฅ Elizabeth Malima Guest Feb 16, 2021
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
๐Ÿ‘ฅ Chris Okello Guest Nov 30, 2020
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
๐Ÿ‘ฅ Lydia Mzindakaya Guest Oct 11, 2020
Kwa Mungu, yote yanawezekana
๐Ÿ‘ฅ Agnes Lowassa Guest Jun 6, 2020
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
๐Ÿ‘ฅ Carol Nyakio Guest Jun 2, 2020
Wakati wa Mungu ni kamilifu
๐Ÿ‘ฅ Faith Kariuki Guest Feb 8, 2020
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
๐Ÿ‘ฅ Stephen Mushi Guest Jan 27, 2020
Endelea kuwa na imani!
๐Ÿ‘ฅ James Mduma Guest Jan 14, 2020
Baraka kwako na familia yako.
๐Ÿ‘ฅ Carol Nyakio Guest Oct 20, 2019
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
๐Ÿ‘ฅ Rose Lowassa Guest Aug 2, 2019
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
๐Ÿ‘ฅ Betty Cheruiyot Guest Jun 7, 2019
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
๐Ÿ‘ฅ Kevin Maina Guest May 19, 2019
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
๐Ÿ‘ฅ Hellen Nduta Guest Dec 25, 2018
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
๐Ÿ‘ฅ Grace Mligo Guest Oct 5, 2018
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
๐Ÿ‘ฅ Daniel Obura Guest Apr 5, 2018
Mungu akubariki!
๐Ÿ‘ฅ Catherine Naliaka Guest Mar 13, 2018
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
๐Ÿ‘ฅ Vincent Mwangangi Guest Jan 5, 2018
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
๐Ÿ‘ฅ Mariam Hassan Guest Nov 27, 2017
Mwamini katika mpango wake.
๐Ÿ‘ฅ Ann Awino Guest Sep 1, 2017
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
๐Ÿ‘ฅ Janet Wambura Guest Jun 24, 2017
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
๐Ÿ‘ฅ Stephen Amollo Guest Apr 11, 2017
Nguvu hutoka kwa Bwana
๐Ÿ‘ฅ Michael Mboya Guest Mar 27, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
๐Ÿ‘ฅ Andrew Mchome Guest Sep 30, 2016
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
๐Ÿ‘ฅ Lydia Mzindakaya Guest Aug 21, 2016
Rehema zake hudumu milele
๐Ÿ‘ฅ George Ndungu Guest Aug 11, 2016
Dumu katika Bwana.
๐Ÿ‘ฅ Elizabeth Mtei Guest Jun 25, 2016
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
๐Ÿ‘ฅ Sarah Achieng Guest May 3, 2016
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
๐Ÿ‘ฅ Anna Malela Guest May 3, 2016
Tembea kwa imani, si kwa kuona
๐Ÿ‘ฅ Moses Mwita Guest Apr 11, 2016
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
๐Ÿ‘ฅ Joyce Mussa Guest Sep 16, 2015
Neema na amani iwe nawe.
๐Ÿ‘ฅ George Ndungu Guest Sep 15, 2015
Tumaini ni nanga ya roho
๐Ÿ‘ฅ Mary Kendi Guest Aug 21, 2015
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
๐Ÿ‘ฅ Kenneth Murithi Guest Jun 20, 2015
Imani inaweza kusogeza milima

๐Ÿ”— Related Posts

๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About