Watu wenye ualbino hawana uwezo kabisa au wana uwezo mdogo wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele na macho. Rangi hii huitwa “melanini”. Rangi ya ngozi itategemeana na kiasi cha melanini kilichopo. Hali ya kuzalisha melanini imekaa katika vinasaba vyetu. Kama vinasaba vya kutoa melanini havipo au vimebadilishwa madhara yake ni ukosefu au upungufu wa rangi. Kwa hiyo hali ya ualbino ni ya kurithi. Inaweza kurithishwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto.