Kuna aina nyingi za unyanyasaji wa jinsia na unaweza kutokea kwa wote wanaume na wanawake. Kwa kawaida unajulikana kama matumizi ya makusudi ya kutumia nguvu na uwezo na kutishia au kwa hali halisi kinyume cha mtu au kikundi au jamii ambapo matokeo yake yanaweza kuleta jeraha au kifo, kuumia kisaikilojia, kutokukua au kudumaa.7 Chini ya sheria za Tanzania8 unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na maneno, sauti ishara au maonyesho ya sehemu za mwili kwa makusudi kinyume na matakwa ya mtu. Hakuna mtu anayeruhusiwa kujamiiana nawe bila ya ridhaa yako, maana hii itakuwa ni ubakaji. Kumlazimisha mtu kujamiiana nawe kwa kubadilishana na zawadi au kumpa kazi ni unyanyasaji wa kijinsia. Kadhalika hakuna mtu anayeruhusiwa kushika viungo vya siri vya uzazi, au kukupiga busu bila ya ridhaa yako. Tendo la ukeketaji ni aina nyingine ya ukatili wa kijinsia. Aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na kumwita mtu majina, kumlazimisha mtu kuvua nguo mbele za watu au kumlazimisha mtu kujamiiana na mtu mwingine. Fikiria kwamba unyanyasaji wa kijinsia ni tendo baya kwa haki za binadamu na unasababisha maumivu kwa wahusika. Tukumbuke kwamba uhusiano wa kimapenzi na watu waliokaribu nasi kwa mfano baba, mama, kaka, dada, babu au bibi ni aina nyingine ya unyanyasaji wa jinsia. Inajulikana kama kujamiiana kwa maharimu “incest“ na inakatazwa kisheria.