Zuzu kaniuliza, "Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana." Nikashtuka, "Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!" Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. "Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti." Nikashusha pumzi. "Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!" Zuzu akanitupia swali. "Kwani we anko ulidhani nini?"