Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive. Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele wa pishori (basmati) - 4
Vitunguu katakata - 3
Nyanya (tungule) katakata vipande vikubwa - 3 -5
Pilipili boga la kijani (capsicum) katakata
Supu ya kitoweo au vidonge vya supu - 1
Bizari mchanganyiko Garama masala - 5-7
Pilipili mbichi ya kusaga - Kiasi
Zaafarani ya maji (flavor) - 1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka mchele kiasi nusu saa kisha chemsha mchele kwa supu uive nusu kiini. Mwaga maji chuja. Wakati mchele unapikika, weka mafuta katika sufuria kubwa ya kupikia wali, kaanga vitunguu mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi. Tia nyanya na vitu vinginevyo vyote kaanga kidogo tu. Mwaga wali katika sufuria na nyunyizia zaafarani kisha changanya na masala vizuri. Funika upike katika oven (bake) au juu ya stovu moto mdogo mdogo kiasi dakika 15- 20. Epua ikiwa tayari, pakua kwenye sahani kisha tolea kwa samaki wa kukaanga.
Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe 2 ¼
Siagi 250g
Sukari kukaribia kikombe ½ (au takriban vijiko 10 vya kulia)
Baking powder ½ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.
MATAYARISHO
Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando. Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo. Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri. Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge. Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa. Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 – 190 deg F kwa takriban robo saa. Epua zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Njia za kupima Afya
Njia mbalimbali hutumika kupima hali ya lishe, njia hizi ni;
1. Vipimo vya umbile la mwili
2. Vipimo vya maabara
3. Kuchukua historia ya ulaji na maradhi
Vipimo vya umbile la mwili
Baadhi ya vipimo ambavyo vinaweza kutumika kutoa tahadhari kuhusu magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni;
1. Uwiano wa uzito na urefu au Body Mass Index (BMI).
2. Mzunguko wa kiuno.
3. Uwiano wa mzunguko wa kiuno na nyonga.
4. Kulinganisha uzito na umri.
Uwiano wa uzito na urefu au Body Mass Index (BMI).
Hiki ni kipimo kinachotumika kuangalia uwiano wa urefu na uzito wa mtu, ni muhimu kuchukua vipimo kwa usahihi.Uwiano wa uzito katika Kilogramu na urefu katika mita hupatikana kwa kutumia kanuni ifuatayo:
BMI= uzito (Kg)/Urefu2 (m2)
BMI huwa na viwango mbalimbali vilivyowekwa na shirika la Afya duniani (WHO) kutafsiri hali ya lishe ya mtu ambavyo ni
1. BMI chini ya 18.5 = uzito pungufu.
2. BMI kati ya 18.5 mpaka 24.9= uzito unaofaa.
3. BMI kati ya 25.0 mpaka 29.9 = unene uliozidi.
4. BMI ya 30 au zaidi = unene uliokithiri au kiribatumbo.
Mahitaji ya chakula mwilini hutegemea umri, jinsi, hali ya kifiziolojia (kama ujauzito na kunyonyesha), hali ya kiafya, kazi na mtindo wa maisha. Uzito wa mwili hutegemea na chakula unachokula, pamoja na shughuli unazofanya, mara nyingi unene hutokana na kula chakula kwa wingi. Unene uliokithiri unachangia kwa kiwango kikubwa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo kubwa la damu, na saratani. Uzito uliozidi unapaswa kupunguzwa ili kuepuka magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza
Jinsi ya kupunguza unene uliozidi
1. Tumia mafuta kwa kiasi kidogo kwenye chakula
2. Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi hususani vinavyopikwa kwa kudumbukizwa kwenye mafuta, au vinavyokaangwa kwa mafuta mengi.
3. Epuka matumizi ya vinywaji au vyakula venye sukari nyingi
4. Epuka asusa zenye mafuta mengi au sukari nyingi kati ya mlo na mlo.
5. Ongeza vyakula venye makapi- mlo kwa wingi kama matunda, mboga mboga na nafaka zisizokobolewa.
BMI haitumiki kwa wanawake wajawazito, BMI haitumiki kwa watoto na vijana walio na umri chini ya miaka 18, BMI haitumiki kwa watu wasioweza kusimama vyema, waliovimba miguu, na wanawake wanaonyonyesha katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua.
Updated at: 2024-05-25 10:35:26 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO
Unga wa mchele 500g
Samli 250g
Sukari 250g
Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai
Baking powder 1 kijiko cha chai
Mayai 4
Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA
1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kupika Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Viazi - 3
Nyama ya Kusaga - 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu - 1 Mug
(Frozen vegetable)
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 1
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 1 vijiti
Karafuu - 3 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Maji - 2 ½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele. Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive. Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu. Tia mboga ya barafu (frozen vegetables) Tia maji, kidonge cha supu. Yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.