Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele (rice vikombe 2 na 1/2) Vitunguu (onion 2) Nyanya ya kopo (tin tomato kopo 1) Tangawizi (ginger paste kijiko 1 cha chakula) Kitunguu swaum (garlic paste kijiko 1 cha chakula) Paprika (kijiko 1 na 1/2 cha cha chai) Pilipil (scotch bonnet pepper 1) Curry powder (kijiko 1 cha chai) Maggi cubes 3(unaweza kutumia yenye ladha ya chicken, beef au vegetable. Inategemea unasevu na mchuzi wa aina gani) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka mchele kwa muda wa dakika 10.Katakata vitunguu kisha weka pembeni, saga pamoja nyanya ya kopo,pilipili, tangawizi na kitunguu swaum kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikiiva tia curry powder, maggi cubes, chumvi na paprika na uchanganye vizuri. Kisha tia mchanganyiko wa nyanya na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia mchele na maji na uupike mpaka ukaribie kuiva kisha ugeuze na umalizie kwa kutia njegere na umalizie kuupika mpaka uive. baada ya hapo utakuwa tayari kuseviwa na mboga yoyote kama kuku, nyama, samaki au assorted meat (Mchanganyiko wa utumbo, makongoro na nyama), Hapo mimi nili-save na mchuzi wa kuku wa kienyeji.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ¾ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ¼ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - ½ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Vanilla ½ kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.) Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Kaanga kitunguu kikishaiva tia nyanya na chumvi. kaanga mpaka nyanya ziive kisha tia nyanya chungu,curry powder na pilipili 1 nzima, baada ya hapo tia mchicha na uuchanganye vizuri kwa kuugeuzageuza. Mchicha ukishanywea tia tui la nazi na uache lichemke mpaka liive na hapo mchicha utakuwa tayari. Safisha nyama kisha iweke kwenye sufuria na utie chumvi, tangawizi, limao na kitunguu swaum. Ichemshe mpaka itakapoiva na kuwa laini. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na mafuta kidogo yakisha pata moto tia vitunguu na nyama na uvikaange pamoja, kisha tia curry powder na ukaange mpaka nyama na viunguu vya brown. na hapo nyama itakuwa imeiva. Malizia kwa kupika wali kwa kuchemsha maji kisha tia mafuta, chumvi na mchele na upike mpaka uive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu
Nyama nyekundu
Hutokana na ng’ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.
Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu. Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : -
• Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata). • Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k. • Kula nyama pamoja na papai
Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.
Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe 2 ¼
Siagi 250g
Sukari kukaribia kikombe ½ (au takriban vijiko 10 vya kulia)
Baking powder ½ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.
MATAYARISHO
Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando. Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo. Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri. Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge. Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa. Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 – 190 deg F kwa takriban robo saa. Epua zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Hoho la kiajani 1/2 Njegere 1 kikombe cha chai Carrot 1 kubwa Broccoli kidogo Cauliflower kidogo Kitunguu 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry power 1 kijiko cha chakula Coriander powder 1 kijiko cha chai Tarmaric 1/2 kijiko cha chai Olive oil Chumvi 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (nusu kilo) Sukari (Kikombe 1 cha chai) Chumvi (nusu kijiko cha chai) Hamira (kijiko kimoja cha chai) Yai (1) Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula) Butter (kijiko 1 cha chakula) Hiliki (kijiko1 cha chai) Maji ya uvuguvugu ya kukandia Mafuta ya kuchomea
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri. Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 ½ gilasi
Sukari ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.