Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
1.💥Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.💥Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.💥 Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
Updated at: 2024-05-23 16:07:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1.💥Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.
2.💥Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.
3.💥 Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!
4.💥Umeweka mbele zaidi "watu watanichukuliaje" kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.
5.💥Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia. 6.💥Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema "umefulia"
7.💥Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.
8.💥Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.
9.💥Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni "Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe" Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi "life skills" wala ujuzi mwingine.
10.💥Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.
ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali. 2.Sponji zenye urembo mbalimbali. 3.Brash kubwa/ndogo. 4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili. 5.Sufuria. 6.Vitambaa vya mpira. 7.Misumari midogo. 8.Jiko.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo
MAHITAJI:
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali. 2.Sponji zenye urembo mbalimbali. 3.Brash kubwa/ndogo. 4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili. 5.Sufuria. 6.Vitambaa vya mpira. 7.Misumari midogo. 8.Jiko.
MADAWA:
1.Sodium hydrosulphate. 2.Caustic soda 3.Mshumaa.
KAZI ZAKE:
1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.
2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.
JINSI YA KUTENGENEZA.
(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:
Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.
(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:
Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.
(c)KUWEKA RANGI YA PILI:
Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,
Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.
(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:
Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji. PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.
"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"- OPRAH WINFREY!
"Sikumaliza elimu yangu ya Chuo Kikuu lakini mimi ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani" - BILL GATES!
"Nilikuwa napata matokeo mabaya sana darasani wakati nilipokuwa shule ya msingi lakini bado mimi ni Daktari Bingwa wa Upasuaji duniani" - DR. BEN CARSON!
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"- OPRAH WINFREY!
"Sikumaliza elimu yangu ya Chuo Kikuu lakini mimi ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani" - BILL GATES!
"Nilikuwa napata matokeo mabaya sana darasani wakati nilipokuwa shule ya msingi lakini bado mimi ni Daktari Bingwa wa Upasuaji duniani" - DR. BEN CARSON!
"Nilimwambia baba yangu tutakuwa na mali na utajiri mkubwa lakini hakuamini, leo hiyo ndiyo hali halisi" - CHRISTIANO RONALDO!
"Nilikuwa mhudumu kwenye mgawahawa wa chai ili kulipia ada za mafunzo yangu ya mpira lakini leo mimi ni mchezaji bora wa dunia" - LIONEL MESSI!
"Nilikuwa nalala chini kwenye vyumba vya marafiki zangu, natafuta chupa tupu za soda nipate chakula, pesa na mlo wa bure wa kila wiki lakini bado mimi ndiye mwanzilishi wa APPLE" - STEVE JOBS!
"Walimu wangu waliniita mwanafunzi mjinga na asiyejiweza lakini bado nimekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza" - TONY BLAIR!
"Niliendesha TAKSI ili kulipia ada yangu Chuo Kikuu lakini leo mimi ni Bilionea" - MIKE ADENUGA!
#NOTE: Kushindwa au Vikwazo vya nyuma ni mambo yasiyo na nafasi kwa UWEZO mkubwa uliomo ndani yako. Kwa mtu anayeamini, kila kitu kinawezekana. Ni tunu ulizonazo na talent ulizopewa ndizo ufunguo wa maisha yako. Usiende kukopa shaba kwa jirani wakati umeacha dhahabu nyumbani kwako, tumia dhahabu zako
Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.
Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?
Updated at: 2024-05-23 16:07:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.
Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?
Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24??? Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyo….katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.
Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk. Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi? Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?
Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24?? Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea. Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.
Kwa maana nyingine kwa kutumia hii "concept" kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio "productive". Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6…kwa maana nyingine kwa "the same concept" ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.
Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive?? Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.
Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio "productive" ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi? Ili uweze kujenga biashara ambayo ni "strong" inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employment…..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??
Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri. Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history. Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.
Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako. Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.
Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.
Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.
Rafiki yawezekana umeshajidharau… na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani… na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.
Updated at: 2024-05-23 16:06:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.
Rafiki yawezekana umeshajidharau… na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani… na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.
Embu ondoa dhana ya kushindwa na kujidharau katika kila hatua upitiayo maishani haijalishi umeshindwa mara ngapi, jifunze kuwa na moyo mgumu na wa subila kwa kila hatua upitiayo maishani,, haijalishi upo katika hali gani? Maishani.
Kama ni maskini sana, usijidharau na umaskini wako ukaona wewe ni wa hali hiyo hiyo maisha yako yote,, no.. hapana, haukuumbwa ili uje kuwa maskini. Ila ni juhudi zako mwenyewe ndizo zitakazokutoa katika umaskini ulionao, haijalishi wewe una ulemavu wa aina yeyote ukajidharau na kujiona huwezi fanya lolote mbele ya jamii likakubalika.
Rafiki kuna walemavu kama wewe, wamejitambua na wameamua… hakika wamefikia mafanikio makubwa maishani. Ondoa dharau katika nafsi yako amini unaweza. Kuna walioshindwa kama wewe wakadharauliwa na kutemewa mpaka mate… ila walitambua kusudi la maisha yao na leo hii wamefikia mafanikio makubwa sana maishani, kwa nini?? Wewe ukate tamaa na kujidharau katika hali uliyopo ukajiona hauna maana? Hakika unaweza ukiamua,
kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..
pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka.. kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka..
Updated at: 2024-05-23 16:07:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Figisu ya Leo. UMESHAWAHI KUFANYA HILI JARIBIO.?
kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake..
pindi inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka.. kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka.. SWALI; NINI KIMEMUUA CHURA.!?? Najua utaniambia ni maji ya moto… La hashaa.! kilichomuua chura ni kushindwa kufanya maamuzi mapema ya kutoka katika chombo cha maji yanayochemka hali ya kuwa bado nguvu anazo.. FUNZO Fanya maamuzi sahihi sasa kabla nguvu za kutaka kufanya changes hazijakuishia kama yaliyomkuta chura.. NOTE; Kuvumilia jambo usiloliweza ni sifa ya punda. BADILIKA.
Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Updated at: 2024-05-23 16:07:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo kwa muda mrefu yamkini unaona panakufaa and you are settled lakini ukweli ni kwamba sio pako na haukutengenezwa kuwa hapo. Hata kama tai ataonekana kwenye banda la kuku lakini ukweli ni kwamba tai kaumbiwa kuwa angani tofauti na kuku aishie bandani. Jiulize hapo ulipo ni pako??
Na ndio maana kwenye maisha, mafanikio ya leo ni matokeo ya tulichojifunza kutoka kwa waliopita, baada ya wao kukosea mahali nasi tukaboresha, na kwa hakika vizazi vijavyo navyo vitaendelea kurekebisha pale tunapokosea sisi na hii yote ndiyo huleta ladha ya maisha. Ukipitia Changamoto mwenyewe na ukapambana kujikwamua mwenyewe, utapata somo litakalokufunza zaidi kuliko kusimuliwa changamoto walizopiti wengine.
Maisha ni Maamuzi, aliyekula Sahani mbili za wali mchana ili usiku asile tena, anaweza kuwa sawa na aliyeamua kutokula Mchana ili usiku ale sahani mbili za wali, japo hawa hawawezi kuwa sawa sawia na aliyeamua kula sahani moja ya wali mchana na moja ya wali usiku, Ijapokua mwisho wa siku wote wamekula sahani Mbili za wali kwa siku. Jumapili Njema kwenu nyote.
Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..
-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?
Kwa sababu ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoka dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)
Updated at: 2024-05-23 16:07:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..
-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?
Kwa sababu ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoka dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)
Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu…!
1. wapo wenye muda wa kutosha Lkn hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)
2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa)
3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia) Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?
Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.
4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..
Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..? Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)
Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..
-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa AU usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zake…!
Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka. 👇👇👇👇👇 Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Updated at: 2024-05-23 16:07:25 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka. 👇👇👇👇👇 Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.
Kazi Mara nyingi napenda kuifananisha na Ndoa, watu wengi walio nje ya kazi wanataka sana kazi na wakidhani ndiyo itakuwa mwanzo wa mafanikio yao.
Vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa ajira wanatamani waingie huko, lakini kutokana na ukweli kwamba kuna vitu hawavijui katika kazi ya kuajiriwa na ndio maana wanajihisi Wanyonge kwa kuto kuajiriwa.
USHAURI kwanza tambua kukosa ajira siyo mkosi, wala siyo kwamba huna bahati. Yawezekana kwakukosa kwako ajira ni mlango wa kuwa muajiri. Unachotakiwa usilalamike tafuta fursa hapo ulipo, ndipo pana utajiri.
1. Kama hujaariwa acha kutamani maisha ya watu walio ajiriwa, ikiwezekana sitisha hata kupiga misele kwenye ofisi, zao kugongea maji ya dispenser
Badala yake anza kutafiti kwakina ni kwa namna gani watu ambao hawajaariwa wanaishi mtaani. Kuwa na marafiki wengi zaidi wanao pambana mtaani ili ujue wao wamewezaje. Tafuta ndege unao fanana nao
2. Usidanganye kwamba ajira ndiyo itajibu matatizo yako yote unajidanganya
Badala yake kama utafanikiwa kupata iyo ajira, hakikisha unaifanya mbegu. Anza kwakuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji maana mshahara hauto kutosha kuishi maisha uliyo nayo kwenye akili yako.
Mwisho kabisa Nguvu na imani uliyoweka kwenye ajira iweke hivyo hivyo kwenye shughuli zako binafsi