Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tezi dume kila mwanaume anazaliwa nayo ambayo inasaidia kutoa maji maji ambayo yanaweza kusaidia kutengeneza mbegu za kiume.
Maji maji hayo yana alkaline ambayo husaidia Wakati Wa tendo la ndoa asidi (acid) iliyopo Kwa mwanamke isiue mbegu za kiume.
Kwahiyo alkaline ikichanganyika na asidi tunapata neutral na hivyo kusaidia mbegu za kiume zisife zinapoingia Kwa mwanamke.
Kwenye uke kuna asidi ambayo inaua kila bacteria wanaoingia.
Acid+base=salt+water
Tezi dume endapo itakuwa zaidi ndo huweza kuleta madhara ambayo ni kufunga mkojo usitoke kwani hubana mrija unaotoka kwenye kibofu kwenda nje.
Tatizo hilo huwakumba zaidi wanaume zaidi ya miaka 50,60,80 japo sio wote.
Kinga yake. 1. Kunywa maji ya kutosha. 2. Kupunguza kula nyama nyekundu. 3. Kupunguza ulaji wa mafuta. 4. Kula matunda na mbogamboga. 5. Kushiriki tendo la ndoa angalau Mara moja au mbili Kwa wiki ili kupunguza maji maji kwenye tezi dume. 6. Kufanya mazoezi ya viungo.
Kwahiyo tezi dume ni kiungo ambacho wanaume huzaliwa nacho isipokuwa kinaleta madhara endapo kitakuwa kupita kiasi na hutibiwa na kupona.
Matibabu yake ni kufanya upasuaji na kupunguza ukubwa pamoja na kudhibiti homoni za ukuaji wake.
Tiba nzuri ya tezi dume ni kufuata ushauri hapo juu na si vidole
Updated at: 2024-05-25 10:35:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ili uweze kuwa na siku nzuri basi unashauriwa kuanza siku yako kwa kutumia mchanganyiko wa maji ya uvuguvugu, asali mbichi, tangawizi, pamoja na limao.
Unashauriwa kutumia mchangayiko huu nyakati za asubuhi mara tu unapoamka ili kupata faida zifuatazo;
1. Husaidia kuyeyusha mafuta mwilini hivyo husaidia kupunguza uzito.
2. Ni kinga ya dhidi ya U. T. I Kwani mchanganyiko huu husafisha kibofu cha mkojo.
3. Husaidia kuupa mwili nguvu.
4:Huchochea mmengenyo wa chakula
Kunywa walau glasi mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.
PROSTATE GLAND (TEZI DUME) TATIZO SUGU KWA WANAUME
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
-Hii ni tezi ya wanaume yenye sifa zifuatazo. ~Ina umbo km yai(oval shape) ~Ina ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume. ~Tezi hii ipo inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje(urethra) ~Tezi hii hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri. ~Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume(shahawa)
SEHEMU KUU ZA TEZI YA KIUME
1.PERIPHERAL ZONE(SEHEMU YA NJE) ~Hii ni sehemu ya nje ya tezi ambayo madakari wengi hutumia hii tezi kubaina kama kuna tatizo kwenye tezi kwani ni virahisi kiugusa km daktari akiingiza ikiingiza index fingure(kidole cha kusontea) kwenye njia ya haja kubwa. Kukua kwa sehemu hii hakuwezi kuathiri utokaji wa mkojo. 2. TRANSITIONAL ZONE(SEHEMU YA KATI) ~ Hii ni sehemu ya tezi ambayo ikikua yani ikiongezeka ukubwa tunasema KUVIMBA KWA TEZI TUME kitalamu BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH) kuna uwezekano mkubwa wa tezi dume iliyovimba kuzuia njia ya mkojo kupita. Kwani ndio sehemu ya tezi iliyo karibu kabisa na njia ya mkojo. Mara nyingi hii sehemu ikikua ndio inayo sababisha matatizo ya kukojoa(obstructive symptoms). Tezi hii pia daktari anaweza kuibaini kwa kutumia kidole kipomo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION(DRE) hii ni kwa sababu ikikua inasukuma ile sehemu ya pembezoni yani peripheral zone kuelekea njia ya haja kubwa. Hivyo dakatri anaweza kubaini km tezi imekua au laa. 3. CENTRAL ZONE(SEHEMU YA KATI) ~Hii sehemu iko mbele ya transitional zone hivyo uvimbe katika sehemu hii ni vigumu kubaini kipitia kipimo hiki cha haraka cha kutumia kidole hivyo tunatumia vipomo vya picha kinaitwa CYTOSCOPY. Hiki ni kipimo cha picha kinacho angalia kipofu cha mkojo na njia ya mkojo na kutoa majibu katika mfumo ya picha au video.
KUKUA KWA TEZI YA KIUME ~Kukua kwa tezi ya kiume kitalamu tunaita BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH). Hili tatizo mara nyingi huanza baada ya miaka 40 hivi na dalili huja kujionesha uzeeni. Hivyo tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili hii ni kutokana na sehemu gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka. Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo ni sugu na liko ktk hali mbaya.
DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI 1. Kukojoa mara kwa mara 2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu 3. Kukujoa sana usiku 4. Maumivu wakati wa kukojoa 5.Kupungukiwa nguvu za kiume 6. UTI ya mara kwa mara 7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo. 8. Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo(hydronephrosis) 9. Kupoteza fahamu(uremia) HIZI DALILI NIMEZITAJA KULINGANA NA TATIZO LINAVYOKUWA SUGU KWA MGONJWA HIVYO UGONJWA HUU NI HATARI USIPO WAHI.
JINSI YA KUBAINI KUVIMBA KWA TEZI ~Kumbuka BPH sio kansa ni uvimbe tu wa kawaida wa tezi lkn kumbuka tezi hii inaweza kuvimba pia kutokana na kansa ya tezi dume (prostate cancer) 1. Uchunguzi wa kawaida kwa kutumia kidole kupitia njia ya haja kubwa kuangalia kama tezi ina tatizo. Kipimo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION. Baada ya kipimo hicho daktari huandika alicho kigusa kama ni ugonjwa au iko kawaida. 2. Hiki ni kipimo cha kupiga picha kibofu cha mkojo kinaitwa CYTOSCOPE. Kumbuka kipimo hiki una ingiziwa waya flani wenye tochi mbele kwenye njia ya mkojo huku huo waya umeunga nishwa kwenye screen. Hivyo chochote huo waya utakacho murika kitaonekana kwenye screen. Ubaya wa hiki kipimo ni kwamba kinaweza kuumiza kuta za njia ya mkojo na baada ya wiki km mbili njia inaweza kuziba mbili jeraha linapo pona. Ila ni kipimo kizuri sana. 3. Kipimo kingine kinaitwa RECTAL UTRASOUND hiki ni kipimo cha kupiga picha kupitia njia ya haja kubwa (rectal) na kutoa picha kwenye jarida gumu kumsaidia daktari kusoma. 4. Kipimo cha kutofautisha kati ya uvimbe wa kawaida(BPH) na kansa ya kipofu(PROSTATE CANCER) Kipimo hiki kinaitwa PROSTATIC SPECIFIC ANTIGEN. Hii ni protein inatolea kwa wingi endapo kuna kansa ya tezi dume. Hivyo damu ya mgonjwa itachukuliwa na kupekwa maabala kuchunguza km ni nyingi kupita kiasi kwenye damu. Kama hii protein ipo kawaida basi uvimbe huo sio kansa ni BPH. Lakini km kiwango ni kingi uvimbe huo ni KANSA. Hivyo uchunguzi zaidi unahitajika kama kuchukua sample ya kinyama kutoka katika tezi na kupeleka maabala.
MATIBABU YA KUKUA KWA TEZI DUME
1. Tezi dume kama haina dalili zozote mara nyingi waga haishighulikiwi sana hospitali lakini dawa za kupunguza kasi anaweza pewa mgonjwa. Lakink ni mara chache. 2. Kama tezi imesha anza kuleta dalili kama usumbufu wakati wa kukojoa siku hizi kuna operation ya bila kukata inaitwa TRANSURETHRAL RECTIONING OF PROSTATE AU CHANNEL TURP. Hii operation inafanywa kama akiwa anafanya kipimo cha CYSTOSCOPE. Lakini hapa anaweka wire mbele kiko chamviringo kinapitishwa njia ya mkojo kina enda kukata kinyama kinachoziba i mean tezi iliyovimba. Hapa inazibua njia ya mkojo ili mtu akojoe. Ukifanyiwa operation hii vizuri tezi hujirudia baada ya miaka kama 3-5 tangu siku ya operation. MADHARA YA TIBA HII 1. Kukosa uwezo wa kufikia kishindo yani hutoi shahawa(RETROGRADE EJACULATION) wazee wengi hulalamika sana baada ya hii operation hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation. 2. Kuziba kwa njia ya mkojo kutoka na kuumia kwa njia hizo wakati wa kitendo hicho. Panapokua panapona hilo kovu linaziba njia ya mkojo. 3. Operation kubwa ya kuondoa tezi hio hufanyika kwa kufungua kibofu cha mkojo na kutoa hio tezi. Madhara ni mengi sana kuhusu hii bora ile no mbili. Kama unahisi unatatizo ili nione mapema kabla mambo aya jakuwa makubwa zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asubuhi kuhusu ugonjwa wa kisukari. Wataalam waliokua wakitoa mada walikua Prof Endrew Swai na Dr Mohamed Juma. Kwa ufupi wamesisitiza sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu,tumbo kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.
Kadhalika wamesisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa,ikiwamo kula dona badala ya sembe,ulezi,mtama na matunda. Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari,ikiwamo juice,soda pombe na vinginevyo. Na hiyo nikwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida. Vyakula visivyokobolewa vinafaida sana kwani vinachukua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini. Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika, na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika. Tafadhalini tujihadharini kwani mada ilikua ndefu na nzuri sana kwa mustakabali wetu na afya zetu. 1.Mazoezi ni muhimu 2.Vyakula viwe na uasilia wake 3.Mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavyowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi 4. Tubadili mifumo ya maisha yetu,kukaa tu bila kuishughulisha miili yetu. Atakayeona anataka kupata elimu zaidi hao madaktari niliowataja wapo hospitali ya muhimbili kitengo cha tiba ya kisukari. Ufahamu juu ya afya yako binafsi โฆnimeikuta sehemu ๐๐๐๐๐๐
Aina ya mazoezi na umuhimu wa mazoezi kwa wamama wajawazito
Updated at: 2024-05-25 10:35:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake.
Mazoezi wakati wa ujauzito yanasaidia:
1. Kupata usingizi mzuri usiku.
2. Kuondoa stress.
3. Kulegeza na kunyoosha misuli ya uzazi na kuitayarisha kwa kazi ya kujifungua.
4. Kupunguza kichefu chefu(morning sickness) na kiungulia(heartburn)
KUMBUKA:
Wakati unafanya mazoezi hakikisha kuwa husikii maumivi yoyote na ukipatwa na maumivu hakikisha unaonana na daktari haraka iwezekanavyo. Kumbuka usilalie mgongo wakati wa kufanya mazoezi au usifanye mazoezi aina ya jogging (kukimbia) au kuruka ruka (bouncing) na hakikisha mdundo wa moyo (pulse) na temperature yako ya mwili ziko sawa. Kunwya maji mengi kuzuia dehydration na angalia balance yako iko sawa ili kuzuia kuanguka.
Kama ulikuwa unafanya mazoezi kabla ya ujauzito unaweza kuendelea na mazoezi yafuatayo:
Kuogelea
Uzuri wa zoezi hili ni kwamba halihitaji nguvu nyingi linasaidia kurelax na misuli yote ya mwili inafanya kazi. Unaweza kuogelea kwa dakika 20 hadi 35 lakini uchukue break pale utakapoona umechoka au kuishiwa na nguvu au pumzi. Kuogelea pia kunasaidia kupunguza maumivu yatokanayo na miguu kuvimba.
Kutembea
Ni zoezi zuri sana kwa mwanamke mjamzito. Zoezi hili linaweza kufanywa dakika 20 had 35 kwa siku. Zoezi hili linapunguza stress, linasaidia chakula kushuka vizuri na digestion. Pia linasaidia katika kuweka sawa uti wa mgongo. Tatizo la uti wa mgongo kutokunyooka linasababishwa na tumbo kuongezeka na kukosekana kwa balance kwenye mwili. Hiki ni chanzo cha maumivu ya mgongo. Kumbuka kuchuka break na kupumzika pale utakaposikia uchovu.
Kucheza Muziki
Mama mjamzito anaweza kucheza mziki kama zoezi hasa hasa mziki wa belly dancing wa kunyonga kiuno na miziki aina ya salsa. Hii inasaidia katika kulainisha misuli ya uzazi tayari kwa kujifungua, kusaidia kujifungua kwa urahisi na kupona kwa haraka zaidi baada ya kujifungua, kupunguza michirizi ya tumbo(stretch marks) inayojitokeza kwa ajili ya ngozi ya tumbo kuvutwa, pia inasaidia confidence ya mwanamke kujiona bado ana mvuto, kuondoa stress, kusaidia na balance, kupunguza maumivu ya mgongo na kusaidia kunyoosha uti wa mgongo.
Kuendesha baiskeli.
Pia unaweza kuendesha baiskeli ila uangalie balance usianguke na usiendeshe sehemu zenye msongamano wa watu au traffic ikiwezekana tumia baiskeli special za mazoezi ndani ya gym(stationary bikes).