Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kupika tambi ni kama ifuatavyo
VIAMBA UPISHI
Tambi pakti moja
Sukari ¾ kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Iliki kiasi
Maji 3 Vikombe vya chai
Vanilla / Arki rose 1-2 Tone
Zabibu Kiasi (Ukipenda)
JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO
1. Zichambue tambi ziwe moja moja.
2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.
3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.
4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto. 5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.
6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa
Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kambale 2 Nazi kopo 1 Nyanya kopo 1 Vitunguu 2 Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula Giligilani kiasi Limao 1/2 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga ngano vikombc 3 Unga mbegu za mchicha kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Maziwa kikombe 1 Sukari kikombe 1 Blue band kikombe ½ Mayai 10-12
Hatua
• Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike. • Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa. • Ongeza sukari na changanya. • Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike. • Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga. • Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo. • Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo. • Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi 6 Nyama ya ng'ombe (nusu kilo) Viazi mviringo 2 Kitunguu swaum Tangawizi Kitunguu maji Nyanya 1 kubwa Mafuta (vegetable oil) Chumvi Limao Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa