Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7
Nyama ng’ombe ½ kilos
Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Haldi (bizari manjano/turmeric) ½ kijiko cha chai
Tui zito la nazi vikombe 2
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga. Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive. Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine. Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi. Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe vya chai
Siagi - 1 Kikombe cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
VIAMBAUPISHI:SHIRA
Sukari - 2 Vikombe vya chai
Maji - 1 Kikombe cha chai
Vanilla ½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
JINSI YA KUTENGENEZA
Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki. Changanya vizuri isiwe na madonge. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. . Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - ½ kikombe
Mafuta - ½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ngano nzima (shayiri) - 3 Vikombe
Kuku - ½ (3 LB takriban)
Thomu na tangawizi iliyosagwa - 1 kijko cha supu
Pilipili manga ya unga - ½ kijiko cha chai
Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Samli ya moto - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri. Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bamia (okra) 20 Nyanya chungu (garden eggs) 5 Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai Nyanya (fresh tomato) 1 Chumvi (salt) kidogo Pilipili 1/4
Matayarisho
Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - ½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - ½ gilasi
Nazi iliyokunwa - ½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike. Mimina katika bakuli la kiasi. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele basmati, pishori - 3 vikombe
Vitunguu katakata - 2
Nyanya/tungule katakata - 5 takriban
Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi
Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia
Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 2
Chumvi - kisia
Mafuta - ½ kikombe
Maji ya moto au supu - 5 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha na roweka mchele Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange. Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo. Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana. Tia mchele ukaange chini ya dakika moja. Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo. Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau. Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (Spaghetti) Nyama ya kusaga Kitunguu maji Nyanya ya kopo Kitunguu swaum Tangawizi Carrot Hoho Lemon Chumvi Curry powder Mafuta Fersh coriander
Matayarisho
Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.