Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon
Updated at: 2024-05-25 10:37:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele vikombe 3
Karoti 1 ikune (grate)
Mchicha katakata kiasi
Adesi za brown
Kitunguu katakata (chopped)
Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2
Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia
Samli ¼ kikombe
Chumvi kiasi
Vipimo Vya Samaki Wa Salmon
Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa
Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia
Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia
Chumvi kiasi
Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia
Ndimu 1 kamua
Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon
Changanya viungo vyote upake katika samaki. Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake. Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili. Akiwa tayari epua.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali
Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori) Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii. Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia. Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo. Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu. Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau. Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Mapishi ya Wali Mweupe Kwa Mchuzi Wa Kuku Wa Balti
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Kuku 1 mkate vipande vipande
Vitunguu 3 katakata (chopped)
Nyanya 5 zikatekate (chopped)
Tangawizi mbichi ilokunwa au ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Thomu (kitunguu saumu) kilosagwa kijiko 1 cha kulia
Bizari mchanganyiko (garam masala) kijiko 1 cha chai
Jira/bizari ya pilau (cummin powder) kijiko 1 cha chai
Dania/gilgilani ilosagwa (coriander powder) kijiko 1 cha chai
Mtindi/maziwa lala (yoghurt) vijiko vya kulia 4 mjazo au paketi moja ndogo.
Malai ya kupikia (cooking cream) kikombe 1
Kasuri methi (majani makavu ya uwatu/dried fenugreek leaves) 1 kijiko cha kulia
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Chumvi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha kuku vizuri mwache achuje maji. Weka mafuta katika sufuria kaanga vitunguu mpaka vianze kugeuka rangi ya brown hafifu. Kisha tia tangawizi na thomu ukaange. Tia kuku ukaange mpaka ageuke mweupe kisha tia nyanya endelea kukaanga ziwive. Piga mtindi vizuri katika kibakuli uwe nyororo. Epua sufuria weka kando kisha tia mtindi uchanganye vizuri pamoja na kuku. Rudisha katika moto acha uchanganyike na kuku kidogo kisha mwagia malai ya kupikia (cooking cream) Tia kasuri methi/majani makavu ya uwatu yaliyovurugwa. Acha katika moto dakika 1 tu. Epua umimine katika chombo na nyunyizia ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (Spaghetti) Nyama ya kusaga Kitunguu maji Nyanya ya kopo Kitunguu swaum Tangawizi Carrot Hoho Lemon Chumvi Curry powder Mafuta Fersh coriander
Matayarisho
Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.