Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti
Updated at: 2024-05-25 17:57:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya. Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena! Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako? Miaka 26: Wenzio wanaolewa. Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia! Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule anaombea unaweza kupata mchumba Miaka 36: At least pata mtoto mmoja. Miaka 39: We will take care of all the wedding billsβ¦yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu . Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
Updated at: 2024-05-25 17:08:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kaziππ
Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali baraa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.
Updated at: 2024-05-25 18:13:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.
Β
Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
Updated at: 2024-05-25 18:02:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Updated at: 2024-05-25 17:15:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem'bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika "NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU"Β πππΒ Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoΒ *Sipendagi Ujinga mimi* πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½