Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.
Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!
Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.
Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.
Updated at: 2024-05-23 16:07:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji. Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo
MAHITAJI:
1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali. 2.Sponji zenye urembo mbalimbali. 3.Brash kubwa/ndogo. 4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili. 5.Sufuria. 6.Vitambaa vya mpira. 7.Misumari midogo. 8.Jiko.
Updated at: 2024-05-23 16:07:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.
Updated at: 2024-05-23 16:07:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
1. Epuka kugeuza mshahara wako kuwa mali ya ukoo. Kamwe mshahara wako siyo mali ya ukoo. Siku utakapoacha kuufanya mshahara wako mali ya ukoo ndipo siku mshahara huo utakuwa mkubwa! Hapo ndipo mshahara utatosha.
2. Siku utakapokuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya mshahara wako ndipo mshahara wako utakapotosha mahitaji yako ya kila mwezi.
Updated at: 2024-05-23 16:07:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndoto ni nini? Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala ni ndoto ya mchana. Ni kile kitu unachotamani kuja kukipata siku moja kabla hujaondoka duniani Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kuwa Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora, Mwandishi Bora, Mfanyabiashara maarufu. Vile vile unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300, Gari la kifahari sana, Unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki utajiri au kuwa Bilionea,Kutembelea nchi fulani na kadhalika.
Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi. Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.
Updated at: 2024-05-23 16:07:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tafuta fursa kila kona. Tumia kipaji chako. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteΒ - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
Updated at: 2024-05-23 16:07:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Sikia haihitaji ukalishwe chini ndo uelewe, Ukweli ni kwamba unajishughulisha Sana na mambo yasiyo Kuhusu katika mafanikio.wazungu husema mind your own business sasa Sijui huu msemo unauchukuliaje?? Imagine unamjua Ali kiba hadi bafuni kwake, tour zote za mwaka huu unazijua hadi nyingine unataka kumpangia, nikuulize wewe ni mwanamziki??
USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.
Updated at: 2024-05-23 16:07:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Anakuja Mchina anasema anahitaji Pakaπ, ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi wanakijiji wanahaha kusaka Pakaπ, wanawaleta mchina ananunua wote anasepa nao. Anarudi tena anasema vipi, naona wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya 35,000 Pakaπ mmoja, wanakijiji wanaenda deep zaidi msituni, kamata Pakaπ, leta kwa mchina, mchina anasepa nao.
Updated at: 2024-05-23 16:07:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako.
Ni wakati mwingine tena tunaenda kujifunza pamoja juu ya mambo mbalimbali ili tuweze kufikia mafanikio kila siku. Leo tunakwenda kujifunza kuhusu pesa na utajua mambo mengi sana juu ya pesa.
FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha yao yatachukua miaka mingi sana kabla hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia fursa moja tu.
Updated at: 2024-05-23 16:07:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi. Matajiri wote wananunua Assets,lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.
Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA! π₯Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.
Updated at: 2024-05-23 16:07:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"- OPRAH WINFREY!
"Sikumaliza elimu yangu ya Chuo Kikuu lakini mimi ndiye binadamu tajiri kuliko wote duniani" - BILL GATES!
"Nilikuwa napata matokeo mabaya sana darasani wakati nilipokuwa shule ya msingi lakini bado mimi ni Daktari Bingwa wa Upasuaji duniani" - DR. BEN CARSON!
Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Duna Lawrence (78) ni raia wa Togo ambaye alijitosa kwenda nchini Ujerumani kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya 80. Baada ya kufika huko, alipata kazi, akawa muaminifu kwa Bosi wake ili aweze kupata mafanikio.
Baada ya miaka mingi kupita, Duna alirudi nchini mwake kwa mara ya kwanza na akaoa, kisha kurejea tena Ujerumani. Bwana Duna aliendelea kufanya kazi kwa bidii huku mafanikio yake kimaisha yakizidi
Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata
π β
Available in PDF
Updated at: 2024-05-23 16:07:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha.
Updated at: 2024-05-23 16:06:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.
Rafiki yawezekana umeshajidharau⦠na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani⦠na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.