Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
β’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa. RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje? JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, βHuyo nguruwe umeshamuondoa?β Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja