Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Jinsi ya kumlisha n'gombe anayekamuliwa atoe maziwa mengi

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu. Malisho ya ng'ombe wa maziwa ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo. Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Kulisha ng’ombe wa maziwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa mifugo mingine kama kuku na hata binadamu, ng’ombe anahitaji mlo bora yaani kamili.

Vyakula vinavyohitajika kwa ng'ombe wa maziwa

Malisho ya kijani (Majani)

Huu ni mlo mkuu kwa ng'ombe wa maziwa. Mlo ni muhimu na wenye virutubisho. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika. Malisho ya kijani yanatakiwa yawe ya kijani kibichi na machanga, hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua. Hii ina maana kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa. Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho yanatakiwa yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.

Vyakula vya kutia nguvu

Kwa kawaida aina zote za majani ni chanzo kizuri cha vyakula vya kutia nguvu kwa mifugo, kama tuu tu yatalishwa yakiwa bado machanga. Mfano wa Majani yaliyo maarufu kwa malisho ni matete, ukoka, majani ya tembo, seteria na Guatemala. Majani ya mahindi au mtama ni chakula kizuri sana kwa kuwapa nguvu mifugo. Vyakula vingine vinaweza kutokana na aina zote za nafaka, punje za ngano, au molasesi. Vyakula hivi vya kutia nguvu vinatakiwa vilishwe kwa kiasi kidogo.

Vyakula vya Protini

Mimea michanga ina kiasi kikubwa cha protini kuliko mimea iliyokomaa. Mahindi machanga pamoja na majani ya viazi vitamu ni mahususi kwa protini. Mikunde ina protini nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, mabaki ya majani ya maharage, njegere, desmodium na lusina. Majani yanayotokana na mimea kama lusina, calliandra au sesbania ina kiwango kikubwa cha protini pia. Aina nyingine ya vyakula vyenye protini ni mashudu ya pamba, mashudu yaalizeti na soya. Ng’ombe wa maziwa wasilishwe kwa kutumia aina zote za jamii ya mikunde kwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa mchanganyiko wa malisho ili kuepuka matatizo ya kiafya.

Madini

Ng'ombe wa maziwa wanahitaji madini ya ziada. Madini Ni lazima yapatikane muda wote, mfano kama jiwe la chumvi au kama chumvi ya unga ya kuweka kwenye (chakula) pumba. Wanyama wanaokuwa, wenye mimba, na ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji kiasi kikubwa cha madini, mfano calcium na phosphorous kwa kuwa madini mengi yanatoka kwenye maziwa. Madini yanaweza kupatikana katika Mimea ya jamii ya mikunde na mengineyo isipokuwa nyasi. Mimea hii inatoa kiasi kikubwa cha calcium na madini mengineyo.

Chakula cha ziada (mf. Pumba)

Ng'ombe wa maziwa anapewa cha kula cha ziada mfano pumba. Pumba inahitajika kwa ng'ombe lakini kwa kiasi kidogo. Pumba aina ya Dairy meal ina kiwango kikubwa sana cha madini. Lakini ina madhara kwa mifugo endapo wanyama watalishwa kwa kiwango kikubwa. Malisho yanayotokana na majani au nyasi kavu ni lazima yabakie kuwa chakula kikuu kwa mifugo. Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6 za pumba kwa siku kwa ng’ombe mwenye kilo 450. Ni lazima wapewe kwa kiwango kidogo sana, ambacho si zaidi ya Kilo 2 kwa mara moja na kichanganywe na majani. Kuongeza kiwango cha pumba kabla na wakati wa kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la mnyama lizoee.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Namna ya kukabiliana na Magonjwa ya kuku

Hakikisha unamuona mtaalamu wa mifugo mara uonapo dalili zozote za kuumwa kwa mifugo wako. Tenga na... Read More
Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na weng... Read More
Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

<... Read More
Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi... Read More
Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo. ... Read More
Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Mambo Ya Kuzingatia Kuongeza Utagaji Wa Kuku

Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina y... Read More

Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukom... Read More

Kilimo bora cha matikiti maji

Kilimo bora cha matikiti maji

Ili kulima tikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na a... Read More

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng'ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo 8 ya kuzingatia kabla ya kuleta mifugo (kuku, ng'ombe,mbuzi n.k) wapya bandani

Mambo hayo ni haya yafuatayo; 1. Hakikisha unaondoa matandazo yote ndani ya nyumba, 2. Ondoa vyombo ... Read More
Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Ukitaka kuwavutia na kuingiza nyiki kwenye mzinga unatakiwa kufanya yafuatayo;

  1. Tafuta ... Read More
Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mtaalamu wa nyuki

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa m... Read More
Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

Jinsi ya kutunza nyumba ya kuku ili kuzuia magonjwa

1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa ... Read More
📖 Explore More Articles | ✍🏻 Re-Write Articles
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About