Ni kiwango gani cha presha kinapofika ndio huwa maradhi ?
Hakuna kiwango maalum kinachojulikana ambacho ni sawasawa kwa watu wote kikifika ndio kinaitwa maradhi. Kiwango ambacho kwako ndio uzima, basi huenda kwa mwenzako ikawa ni maradhi. Katika presha ya kushuka, madaktari wengi huchukulia kuwa tayari mtu ana maradhi pale aambapo kiwango chake cha presha kinafuatana na dali za maradhi yenyewe. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachukulia tayari mtu ana maradhi ya presha ya kushika pale vipimo vinapoonyesha kiwango hichi 90/60ย mm Hg. Tufahamu kuwa kiwango cha namba inayosomwa chini katika kipimo cha presha (โฆ /60ย mm Hg ), hichi huonyesha tayari mtu huyu anapresha ya chini hata kama kile cha juu ( 90/โฆmm Hg) kina namba iliyozidi 100. Mfano ikiwa umepimwa presha na ukapata kipimo hichi 115/60ย mm Hg, presha yako itakuwa ipo chini. Na kama umepata kipimo hichi 115/50ย mm Hg, sio kwamba presha yako itakuwa ipo chini tu, bali presha hii itakuwa si ya kawaida.Dalili za maradhi
Kama nilivyokwisha tangulia kusema, presha inaweza kuwa sawa kati ya watu wawili lakini ikawa na matokeo tofauti. Presha hiyo inayoweza kuwa sawa na ikawa na matokeo tofauti si yenye kipimo hichi 120/80ย mm Hg. Presha yenye kipimo hichi 120/80ย mm Hg, ndiyo nzuri na watu wenye presha hii wanakuwa na afya nzuri. Kitu muhimu ni kujua, mabadiliko gani yanaleta tatizo katika presha hata inapelekea kuwa si ya kawaida. Presha nyingi za watu wanapopimwa huwa zinakuwa kati ya 90/60ย mm Hg (presha iliyo chini) mpaka 130/80ย mm Hg (presha iliyo juu). Mabadiliko ya kushuka presha upande wa chini, hata kama kidogo kiasi cha 20ย mm Hg, hupelekea matatizo kwa baadhi ya watu ( hasa watu wasiofanya mazoezi kila siku). Mtu mwenye mazoezi ambaye presha yake nzuri (120/80ย mm Hg) akapimwa presha na kupata kipimo hichi, 110/60ย mm au 120/70ย mm Hg, mtu huyu hatakuwa na tatizo lolote la presha Kuna aina tatu za presha ya kushuka : Orthostatic sambamba na postprandial orthostatic (Orthostatic hypotension, including postprandial orthostatic hypotension) Orthostatic, hii ni aina ya kwanza ya presha inayosababishwa na kubadili mazingira uliyonayo kwa ghafla, maranyingi hutokea kwa mtu anayesimama kutoka alipolala. Presha hii haidumu muda mrefu, kiasi cha sekunde chache mpaka dakika moja. Ikiwa presha hii itatokeze. baada ya kula, basi itakuwa ni hatua ya pili (postprandial orthostatic) . Hatua hii ya pili huwapata zaidi wazee na wenye presha ya juu. Neurally mediated hypotension (NMH) NMH kama ilivyo kifupisho cha presha aina ya pili, huwapata zaidi vijana na watoto. Presha hii hutokea pale mtu anaposimama kwa muda mrefu. Maranyingi huwapata sana watoto.Aina hii ya pili ya presha ya kushuka maranyingi husababishwa na hali zifuatazo :
- Utumiaji wa pombe
- Utumiaji wa dawa za kutibu presha ya juu.
- Utumiaji wa dawa za kumtoa fahamu mtu wakati wa kufanyiwa upasuaji
- Ugonjwa wa Kusukari
- Mtu kula kitu kinachomdhuru
- Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
- Maradhi ya kuharisha
- Kuzimia
- Maradhi ya moyo
- Maradhi ya kustuka
- Kuona kizunguzungu/kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa
- Kuzimia
- Kushindwa kuzingatia
- Kushindwa kuona vizuri ghafla
- Kuona baridi,
- Kujihisi kuchoka sana
- Kuvuta pumzi kwa tabu
- Kutapika
- Kuhisi kiu
Hali zinazosababisha kupata presha ya kushuka.
Kinachosababisha presha ya chini bado hakijatambulika hasa. Chanzo chake hakiko wazi. Hata hivyo mambo yafuatayo yanaweza kuhusiswa nayo :- Kuwa na mimba
- Matatizo ya homoni mwilini, maradhi ya kisukari, au upungufu wa sukari mwilini
- Utumiaji mkubwa wa dawa
- Ulaji wa dawa za presha unaopindukia kiwango (Overdose) kwa mtu mwenye presha ya juu.
- Maradhi ya moyo
- Maradhi ya figo
Nani anapata presha ya kushuka ghafla ?
Presha ya kushuka ghafla inayompata mtu anapoinuka ghafla, inaweza kumpata mtu yeyote kwa sababu tofauti zikiwemo,- kuharisha sana,
- kukosa chakula ( njaa kali) kwa muda mrefu,
- kusimama kwa mapigo ya moyo, au
- kuchoka kupita kiasi.
- Pia inawezekana ikawa ni urithi wa maradhi,
- Umri mkubwa,
- Matumizi ya dawa,
- Utapiamlo na mambo mengine kama kupatwa na madhara ya jambo fulani.
Nini kinaifanya presha inayoshuka iendelee ?
Pia Presha ya kushuka mara nyingi huwapata watu wanaotumia dawa kwa kutibu presha ya juu (hypertension). Pia huwapata wajawazito au wagonjwa wa kisukari. Mara nyingi wazee nao hupata maradhi haya hasa wale walio na presha ya juu wakiwa wanaendelea kutumia dawa zao za presha. Baadhi ya maradhi ambayo yanasababisha presha kushuka kuendelea ni pamoja na;- Ukosefu wa vitamin mwilini,
- Madhara kwenye uti wa mgongo, na
- Kansa hasa kansa ya mapafu.
Wakati gani wa kuchukua hatua za matibabu
Matibabu huanza na hatua zako wewe mwenyewe. Wakati utakapojiona presha yako inashuka, kaa chini au lala chali na unyanyue miguu yako juu. Wakati yanafanyika haya, ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari haraka. Pia ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari yanapoonekana mambo yafuatayo yamemkuta mtu :- Maumivu ya kifua
- Kizunguzungu
- Kuzimia
- Homa kali sana
- Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
- Kupumua kwa tabu
- Mtu anapata matatizo makubwa ya mkojo
- Kushinwa kula au kunywa chochote
- Kuendelea kuharisha au kutapika kwa muda mrefu