Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Neno Albino linamaanisha
mtu mweupe, linatokana na
neno la lugha ya Kilatini -
albus-linamaanisha βeupeβ.
Kuanzia karne ya 17 neno
Albino limekuwa likitumika
katika kueleza hali ya kundi
la viumbe hai (watu, wanyama
na hata mimea) ambao wana
upungufu au ukosefu wa rangi
katika ngozi, macho na nywele.
Kwa binadamu ni bora kutumia
maneno βWatu wanaoishi na
ualbino
kwani itamaanisha kuwa ni watu kama wengine ila wanaishi na
hali tofauti ya βualbinoβ. Katika kitabu hiki maneno haya mawili
yatatumika.
Lugha inajenga dhana na kuunda hali ya ukweli / uhalisi. Kwa
sababu hiyo ni lazima tuache kutumia maneno kama βzeruzeruβ.
Neno hili linamaanisha sifuri mara mbili au mtu asiye na
thamani. Utumiaji wa neno hili ni dharau ya utu na kulaumu
watu wanaoishi na ualbino kama kosa lao.