Njia za Kuzuia Mimba
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Date: April 16, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:
Vizuizi
(hizi huzuia mbegu kulifikia yai): Kuna mpira wa kiume (kondomu ya kiume), yaani mfuko wa mpira uliozibwa upande moja. Unavishwa kwenye uume uliosimama kabla ya kuingia ukeni. Pia kuna mpira wa kike (kondomu ya kike), yaani mpira unaoingizwa ukeni kabla ya kujamiiana.
Vidonge vya kuzuia mimba:
Lazima mwanamke anywe vidonge hivi kila siku hata kama hajamiiani.
Njia nyingine za kuzuia mimba kwa muda mrefu
. Njia hizi hazihitaji maandalizi maalum, ili kuzuia mimba, kabla ya kujamiiana na pia mwanamke hahitaji kukumbuka kufanya chochote kila siku. Kati ya njia hizi ni pamoja na sindano anazopewa mwanamke kila baada ya miezi mitatu. Pili, kuna vipandikizi, yaani vijiti vyembamba vya plastiki vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mama kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa yai. Pia, kuna kitanzi ambacho ni kitu kidogo kilichotengenezwa kwa aina maalum ya plastiki. Kwa ufupi kinaitwa IUD. Huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Sindano, vipandikizi na vitanzi lazima viwekwe na mtaalamu mwenye ujuzi kwenye kituo cha afya chenye vifaa vya kutosha. Kwa vile dawa za kuzuia mimba kwa muda mrefu zinaingiliana na mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa kiasi, athari zake ni kubwa kuliko kutumia vidonge.
Kwa mwanaume na mwanamke kuna njia ya kudumu ya kufunga kizazi kwa njia ya upasuaji
. Kwa mwanaume mirija inayopitisha mbegu hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mbegu zisitoke. Akijamiiana, anaweza kumwaga shahawa, lakini ndani ya shahawa hakuna mbegu. Kama mwanaume amefunga kizazi uume utadinda kama kawaida na kufikia mshindo atamwaga maji ya shahawa ambayo hayatakuwa na mbegu. Kwa mwanamke mirija ya kupitisha mayai hukatwa na kufungwa, ili kuzuia mayai kufika kwenye mfuko wa uzazi. Baada ya upasuaji huu, mama ataendelea na hedhi kama mwanzo, lakini yai halitaweza kukutana na mbegu za kiume tena.
Vilevile kuna njia nyingine mbalimbali ambazo hazina uhusiano na matumizi ya dawa au vizuizi vya mimba. Njia hizi hazina uhakika mkubwa wa kutopata mimba. Mara nyingine mama anatumia ishara mbalimbali, au tarehe kujua lini anaweza kupata mimba, ili kuepuka kujamiiana katika kipindi hicho. Kumwaga mbegu za kiume nje ya uke, au kutegemea kwamba mimba hazishiki wakati wa kunyonyesha ni njia nyingine za asili zinazotumiwa. Kumbuka kwamba njia hizi hutumika sana, lakini si njia salama sana za kuzuia mimba wala kuambukizwa na magonjwa ya zinaa.
Ni muhimu kukumbuka kwamba njia ya uzazi wa mpango inaweza kufaa kwa mtu huyu na isifae kwa mtu mwingine. Kwa hiyo, ni vizuri kila mtu aliyeamua kupanga uzazi apate ushauri kwenye kliniki kuhusu njia inayomfaa zaidi
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Leo kwenye makala hii, tutazungumzia vidokezo vya kuwa na mawasiliano ya kuaminika na msichana. N...
Read More
Kama mama mjamzito atatumia dawa za kulevya basi humuathiri mtoto moja kwa moja. Mtoto aliye tumb...
Read More
Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana ...
Read More
Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano
-
Kuwasiliana kwa Ukaribu
Ha...
Read More
Leo tutaongelea kuhusu umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono au kufanya ...
Read More
Urafiki mzuri ni msingi muhimu wa kuanza uhusiano wa kimapenzi. Kujenga urafiki mzuri na msichana...
Read More
Kwa wengi, ngono inaonekana kama kitendo cha kimwili tu bila ya umuhimu wa kujadili mawazo na his...
Read More
Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuing...
Read More
Ndiyo. Unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara au kunywa
pombe. Lakini pale tu utakapozidisha...
Read More
Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa nji...
Read More
Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano? Swali hili ni mo...
Read More
Je, kuna umuhimu wa kujadili matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu kwenye ngono/kufanya mapenzi? B...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!