Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Mambo ya Msingi kuyajua Ili uishi na watu vizuri

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza:-
1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)
2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako)

3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti ukweli (pengine wapo wanadamu wanaopenda kuonekana wao wema kwa kuumiza wengine). Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta.

4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji (tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya).

5. Usipande mbegu ya chuki na ubaya katika jamii unayoishi ukadhani itakuacha salama (chuki hukua kama mti utambaao, ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako na inaweza kutafuna kizazi chako ukajutia.

6. Tambua kuwa yule unayeishi nae ni mwanadamu kama wewe, mpe heshima na mwonyeshee upendo hata kama huoni anafanana nawe. Maisha ni duara huenda ulikuwa kama yeye au atakuja kuwa kama wewe baadae.

6. Usiwe muongeaji ovyo ovyo na usiye na subira. Kuongea sana kunapoteza busara.

7. Jiepushe na maisha ya kusukumwa na wengine kufanya jambo usilojua manufaa yake. Jifunze kujitegemea kiakili. Sio kila unayemdhania rafiki moyoni mwake yupo pamoja nawe, na ukashirikiana nae, wengi wa marafiki zetu hututumia sana kuliko tunavyoweza kuwatumia wao.

8. Usipende sana kugombana na watu kwa njia ya maongezi yanayodumu kama vile, ujumbe wa maandishi, mawasiliano ya simu au ujumbe wa maneno (SMS). Kumbuka kuwa maneno yanaishi kuliko ugomvi au uadui, ipo siku yatakurudi na utajiona mpumbavu na kukosa pa kujificha. Jifunze kusubiri.

9.Usifumbue mdomo wako kutamka ubaya au kunyanyua kidole chako kuandika ubaya juu ya mwenzio bila kujiuliza mara mbili moyoni mwako hatima ya unachokitoa kwa mwingine.

10. Jishushe na jifunze kusikiliza wengine wakati wa mazungumzo ili uweze kujifunza kabla ya kukurupuka kujibu, usikivu ni kipimo cha busara, mtu anayekurupuka kujibu jibu kila anachosikia hawezi kuwa kiongozi, Mume au Mke mwema kwani mara nyingi atapotoka tu.

10. Usitunze hasira nyingi moyoni kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Jitahidi pia kuepuka kuwa na hasira mara kwa mara na zisizo na maana. Elewa kuwa hasira zisizo maana hukupunguzia maisha na kukupa maumivu wewe mwenyewe kuliko yule uliyemfanyia hasira, utakufa kwa magonjwa kabla ya wakati ufaao.

11. Thamani yako inategenezwa na watu wengine, wewe kama ni mtoto, mheshimu sana mzazi wako na kama umeoa au kuolewa, heshimu wazazi na familia ya mke au mumeo kwa kuwa bila wao, usingekuwa hivyo ulivyo leo unajivunia ndoa njema, kwa kuwa yupo mtu alimzaa huyo mwenzio. Mheshimu kwa lolote liwe jema au baya, utalipwa kwa wakati ufaao.

13. Usijibizane na mtu usiyemjua au ambaye hawezi kukupunguzia kitu katika maisha yako. Tambua kuwa unapunguza sehemu kubwa ya maisha yako kwa kutafuta magomvi na mtu wa mbali nawe.

14. Kumbuka asili yako, kumbuka upo hapo kwa kuwa kuna mahali ulitoka, maisha yanabadilika, usidharau pale ulipokuwa zamani kwa kuwa ndipo palipokufanya leo uwe hapo.

15. Subiri, sikiliza, elekeza, vumilia. Elewa sio kila mtu ana uelewa kama wako. Jitahidi kuwa mvumilivu katika kila jambo, usiinuke kuwafokea au kuwakaripia wengine kwa jambo ambalo pengine nao wanahitaji muda kueleweshwa ili walifanye vyema. Kumbuka sana, kuna wakati nawe ulikuwa huelewi kabisa lakini wapo wenzio walikuvumilia, wakakuelekeza njia njema, kufokea wengine mara kwa mara sio njia njema ya kuwafundisha bali ni kuwaweka mbali nawe.

Kumbuka: Ishi kwa kumpendeza Mungu.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na mitazamo na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kisiasa na mitazamo na mpenzi wako

Hakuna jambo zuri zaidi kuliko kumpata mpenzi ambaye mnashirikiana mambo mengi. Lakini, wakati mw... Read More

Njia za Kuimarisha Umoja wa Kifamilia na Kuweka Maadili ya Pamoja

Njia za Kuimarisha Umoja wa Kifamilia na Kuweka Maadili ya Pamoja

Umoja wa kifamilia ni kitu muhimu katika maisha ya kila mmoja wetu. Familia ndiyo kitovu cha mais... Read More

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Ndoa na mke wako

Kuweka malengo ya ndoa na mke wako ni hatua muhimu katika kujenga msingi imara na kufikia furaha na ... Read More
Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kitamaduni katika mtazamo wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari za leo wapenzi wa Kiswahili! Leo tutajadili suala la tofauti za kitamaduni katika mtazamo ... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Mipango ya Pamoja katika Familia

Katika famil... Read More

Mbinu 6 za Kujenga Uhusiano wa Kimwili na Kihisia na mke wako

Mbinu 6 za Kujenga Uhusiano wa Kimwili na Kihisia na mke wako

Kujenga uhusiano wa kimwili na kihisia na mke wako ni muhimu katika kuimarisha ndoa na kuendeleza in... Read More
Uhusiano wa Mbali na Kufanya Mapenzi: Njia za Kuimarisha Ushirikiano wakati wa Kutengana

Uhusiano wa Mbali na Kufanya Mapenzi: Njia za Kuimarisha Ushirikiano wakati wa Kutengana

Muda mrefu wa kutengana na mpenzi wako unaweza kuwa mgumu sana, hasa ikiwa mnatumiana kimapenzi. ... Read More

Jinsi ya Kushughulikia Uaminifu na Udanganyifu wa mke wako

Jinsi ya Kushughulikia Uaminifu na Udanganyifu wa mke wako

Kushughulikia uaminifu na udanganyifu katika ndoa ni suala nyeti na linalohitaji mchakato wa kina. H... Read More
Njia za Kupunguza Mazoea ya Kuigiza katika Kufanya Mapenzi: Kuhamia kwenye Uzoefu Halisi

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kuigiza katika Kufanya Mapenzi: Kuhamia kwenye Uzoefu Halisi

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kuigiza katika Kufanya Mapenzi: Kuhamia kwenye Uzoefu Halisi

K... Read More

Kufanya Mapenzi na Afya: Jinsi yanavyoathiri Mwili na Akili

Kufanya Mapenzi na Afya: Jinsi yanavyoathiri Mwili na Akili

Kufanya mapenzi ni moja ya mambo muhimu katika maisha yetu. Kwa kuwa mapenzi yana athari kubwa kw... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Migogoro ya Familia kwa Ufanisi: Mbinu na Mikakati

Jinsi ya Kukabiliana na Migogoro ya Familia kwa Ufanisi: Mbinu na Mikakati

Karibu kwenye makala hii ya jinsi ya kukabiliana na migogoro ya familia kwa ufanisi. Migogoro ya ... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuwa na Msamaha katika Mahusiano

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuwa na Msamaha katika Mahusiano

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu, lakini mara nyingi tunaweza kuingia kwenye mazo... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles | โœ๐Ÿป Re-Write Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About