Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

Usipoteze muda - jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani - soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

Jenga urafiki na taasisi za kifedha - mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha - tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA

Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.

Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU

Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa - angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA

Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA

Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

Fanya vitu wewe mwenyewe - acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu

Kuwa na malengo - kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT

Kuwa na moyo wa ujasiri - usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA

Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

Acha woga - jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

Kuwa na mtazamo chanya - usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

Kuwa na mipaka katika mambo yako - usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu

Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako - waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe

Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja

Ubunifu ni muhimu sana - fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini - kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli
PIGA KAZI

Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea

Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea - kila binadamu anaweza kuwa milionea

Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa - kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Ila kuthubutu ndo hatua ya kwanza.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

BADILIKA : huu ni mwaka mpya

BADILIKA : huu ni mwaka mpya

**Badilika huu mwaka. Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani ... Read More

Mambo ya kufanya mwezi Disemba

Mambo ya kufanya mwezi Disemba

Ikiwa leo ni tarehe **1/12 huwezi amini kuwa hakuna t... Read More

Ushauri wangu kwa leo

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kus... Read More

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Read More

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho... Read More

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadam... Read More
Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitu... Read More

Nia yako isishindwe

Nia yako isishindwe

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni "NIA".
Nimemtazama mwendesha pik... Read More

FUNZO: Maisha ni kuchagua

FUNZO: Maisha ni kuchagua

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ ... Read More

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hu... Read More

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Hofu inavyo tugharimu katika safari ya ujasiriamali na Jinsi ya kuiepuka

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapeda kuwa kama Mengi siku moja.

... Read More

Ni vizuri kujua haya

Ni vizuri kujua haya

👉🏿Degree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
👉🏿Uzuri ulio nao hauwe... Read More

📖 Explore More Articles
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About