Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Amri ya Kwanza ya Mungu: Mambo Muhimu ya Kuzingatia

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9)


Wakatoliki tunamwabudu Mungu kwa namna gani?

Tunamwabudu Mungu kwa sala , sadaka na matendo mema


Katika amri ya kwanza ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu.


Je, kuna viumbe ambavyo tunaviheshimu kwa kumtukuza Mungu?

Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu.


Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu.


Je, tuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu?

Hatuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu tunawaheshimu tu.


Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.

Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.


Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.


Ni nanai ana kosa kumuabudu Mungu?

Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;

1. Anayeacha kusali au anayesali hovyo
2. Anayemkufuru Mungu
3. Anayeamini na kushika mambo ya kipagani


Mambo gani yanavunja amri ya kwanza ya Mungu?

Mambo hayo ni;

1. Kuabudu sanamu
2. Kufanya matambiko
3. Kwenda kwa waganga
4. Kupiga bao au ramli
5. Kuvaa hirizi
6. Kushiriki mambo ya kichawi n.k.


Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.


Kutokumuabudu Mungu ni kwa namna gani?

Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki.


Mkatoliki anaabuduje?

Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani


Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwaΒ Mkao wa sala


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)

Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;

"18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.Β (Kutoka 25 :18-22.)"

Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?

Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.

"BWANA akamwambia Mose, β€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi."Β (Hesabu 21:8-9).

Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.

Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.

Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.

Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.

Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.

KumbukaΒ kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwaΒ "Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake", kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani:Β Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki:Β Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.Β (Kutoka 25 :22).Β Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale:Β Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hichoΒ Kutoka 25:10-22.Β Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.

Kwenye Agano jipya:Β Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.

FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.

Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tunawaheshimu Watakatifu namna gani?

Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Janet Mwikali Guest Jun 12, 2024
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
πŸ‘₯ Lydia Mutheu Guest Feb 29, 2024
Nguvu hutoka kwa Bwana
πŸ‘₯ Brian Karanja Guest Sep 2, 2023
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
πŸ‘₯ Samuel Omondi Guest Jul 5, 2023
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
πŸ‘₯ George Tenga Guest Jul 1, 2023
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
πŸ‘₯ Isaac Kiptoo Guest Apr 18, 2023
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
πŸ‘₯ Andrew Mahiga Guest Mar 8, 2023
Kwa Mungu, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Mary Kendi Guest Jul 19, 2022
Neema ya Mungu inatosha kwako
πŸ‘₯ Jane Muthui Guest Mar 3, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
πŸ‘₯ Joy Wacera Guest Feb 12, 2022
Baraka kwako na familia yako.
πŸ‘₯ Robert Okello Guest Feb 9, 2022
Mwamini katika mpango wake.
πŸ‘₯ Patrick Kidata Guest Jun 13, 2021
Wakati wa Mungu ni kamilifu
πŸ‘₯ James Kawawa Guest Jan 2, 2021
Rehema zake hudumu milele
πŸ‘₯ Faith Kariuki Guest Nov 21, 2020
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
πŸ‘₯ Mariam Hassan Guest Aug 1, 2020
Endelea kuwa na imani!
πŸ‘₯ Mary Sokoine Guest Jun 27, 2020
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
πŸ‘₯ Elizabeth Malima Guest Apr 24, 2020
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
πŸ‘₯ Elizabeth Mtei Guest Jan 31, 2020
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
πŸ‘₯ Alice Mwikali Guest Jan 11, 2020
Mwamini Bwana; anajua njia
πŸ‘₯ Robert Ndunguru Guest Dec 10, 2019
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
πŸ‘₯ Brian Karanja Guest Nov 26, 2019
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
πŸ‘₯ Patrick Akech Guest Oct 22, 2019
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
πŸ‘₯ Catherine Mkumbo Guest Sep 6, 2019
Mungu akubariki!
πŸ‘₯ Catherine Naliaka Guest Aug 9, 2019
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
πŸ‘₯ Lydia Mzindakaya Guest Aug 8, 2019
Tembea kwa imani, si kwa kuona
πŸ‘₯ Victor Mwalimu Guest May 30, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
πŸ‘₯ Edward Lowassa Guest Apr 24, 2019
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
πŸ‘₯ Joyce Nkya Guest Mar 8, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
πŸ‘₯ George Tenga Guest Jan 29, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Dorothy Mwakalindile Guest Sep 19, 2018
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
πŸ‘₯ Victor Kimario Guest Aug 28, 2018
Dumu katika Bwana.
πŸ‘₯ Dorothy Mwakalindile Guest Apr 20, 2018
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
πŸ‘₯ Kevin Maina Guest Mar 2, 2018
Mungu ni mwema, wakati wote!
πŸ‘₯ Edward Lowassa Guest Nov 30, 2017
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
πŸ‘₯ Victor Mwalimu Guest Nov 16, 2017
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
πŸ‘₯ Lydia Mutheu Guest Oct 10, 2017
Neema na amani iwe nawe.
πŸ‘₯ Henry Mollel Guest Aug 6, 2017
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Alice Jebet Guest Jun 8, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
πŸ‘₯ Nancy Akumu Guest Mar 2, 2017
Sifa kwa Bwana!
πŸ‘₯ Nancy Akumu Guest Dec 25, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
πŸ‘₯ Martin Otieno Guest Nov 7, 2016
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Esther Nyambura Guest Nov 3, 2016
Nakuombea πŸ™
πŸ‘₯ Daniel Obura Guest Oct 20, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Elijah Mutua Guest Aug 26, 2016
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
πŸ‘₯ Grace Njuguna Guest Apr 21, 2016
Rehema hushinda hukumu
πŸ‘₯ George Mallya Guest Apr 19, 2016
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
πŸ‘₯ Francis Njeru Guest Jan 4, 2016
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
πŸ‘₯ Edith Cherotich Guest Dec 11, 2015
Katika imani, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Samuel Omondi Guest Oct 23, 2015
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
πŸ‘₯ Samson Mahiga Guest Sep 11, 2015
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About