Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
β’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, βNi lini mara ya mwisho umemwambia mumeo βNakupenda Mpenziβ?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno βNAKUPENDA MPENZIβ Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 β βSamahani, nani mwenzanguβ! Simu ya 2 β βSamahani, wrong numberβ! Simu ya 3 β βSi nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hiiβ! Simu ya 4 β βMh! leo mvua itanyeshaβ! Simu ya 5 β βNikija tutaongea zaidiβ! Simu ya 6 β ββ¦β¦Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa β¦β¦β! Simu ya 7 β βMe tooβ! Simu ya 6 β βHuu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikomaβ!