Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - ½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - ½ gilasi
Nazi iliyokunwa - ½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike. Mimina katika bakuli la kiasi. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga wa ngano vikombe vikubwa 3 Boga lililopondwa kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Sukari kikombe kikubwa 1 Blue band kikombe ½ Vanilla kijiko kidogo 1 Mayai 2 Maji kiasi/ maziwa (kama nilazima)
Hatua
• Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike. • Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa. • Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa. • Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole. • Ongeza sukari na changanya. • Ongeza mayai na koroga na mwiko. • Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike. • (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo). • Ongeza vanilla na koroga. • Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano. • Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea. • Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive. • Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug
(Frozen veg)
Tuna (samaki/jodari) 2 kopo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi 2 vijiko vya supu
Garam masala 1 kijiko cha supu
Nyanya 2
Kitungu maji 1
Mdalasini nzima 2 vijiti
Karafuu 6 chembe
Pilipili mbichi 1
Chumvi kiasi
Viazi 3
Maji 2 ½ Mugs
Mafuta 3 vijiko vya supu
Jinsi ya kuandaa na kupika
Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20 Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu. Tia maji, yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ¾ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ¼ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - ½ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Vanilla ½ kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.) Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua. Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa.na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula · Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula · Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula · Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi. Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi. Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi. Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi. Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive. Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.