Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
jamaa akagoma kwenda kazini 😬😬 mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwa nimemdhibiti ndo mana hatoki🚷 jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwa ulidhani rafiki yako kumbe adui yako🤔🤔 jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwa ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Updated at: 2024-05-25 17:04:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimeenda mahakamani, mara judge akasema.. Order! Order… Mimi na kiherehere changu nikasema.. Chapati .. Maziwa na ovacado tatu … Nimewekwa kwa karoom kengine hapa kanagiza.. i think wananiandalia chapati 😀😁😀😁😀😁😀😁😂
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endelea…"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endelea…"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaa…. "Padri yesu atanisamehe?" kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu……."
Updated at: 2024-05-25 18:09:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania. Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa: Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha 1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture 2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
Updated at: 2023-04-29 22:53:54 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha 1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture 2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema"Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita"
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Updated at: 2024-05-25 17:06:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??. Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaa… 😂😂