Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:45:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu?
Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu
Updated at: 2024-05-25 17:07:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuβ¦.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπππππππ
Updated at: 2024-05-25 18:10:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza "Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?" Akajibiwa "Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu π³π³π³π³π³
Eti ni kweli hii ni sababu wanaume wana Upendo Sana?
Updated at: 2024-05-25 16:52:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!* Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana ππππππ
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
Updated at: 2024-05-25 18:06:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.
Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni. Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza? Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.
Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita. Bakari:Babaa! Boss: naam Bakari! Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss kimyaaaa! Bakari: Baba babaa! Boss:ndio Bakari! Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss kimyaaaaaaa! Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!
Mke wa Boss akaingilia kati Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje? Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone
Mama akaenda na Bakari akaanza
Bakari: mamaaaa! Mama: abeee! Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu? Mama kimya
Bakari: mamaaaa! Mama: abeeee! Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu?? Mama kimya
Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu
Kilichotokea baada ya bibi na babu kukumbukia mahaba ya ujanani
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Updated at: 2024-05-25 18:02:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoiiβ¦