Viamba upishi
Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ยฝ
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)
Hatua
โข Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike.
โข Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa.
โข Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa.
โข Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole.
โข Ongeza sukari na changanya.
โข Ongeza mayai na koroga na mwiko.
โข Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike.
โข (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo).
โข Ongeza vanilla na koroga.
โข Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano.
โข Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea.
โข Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive.
โข Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!