Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda midomo au sehemu nyeti. Yafuatayo ni mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu Ugonjwa wa Kaswende.

Jinsi ugonjwa wa Kaswende unavyoonea

Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi. Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.

Kwa njia ya Kujamiiana

Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi huambikizwa kupitia ngono. Kwa sababu ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, njia kuu ya kuenea ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile.

Kwa njia ya kugusana Miili

Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.

Kwa mtoto kipindi cha ujauzito

Mwanamke mwenye mimba na ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa. Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua โ€“ hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.

Hatua za Kaswende

Ugonjwa wa kaswende hugawanywa katika hatua na kila hatua ikiwa na dalili tofauti, lakini wakati mwingine hakuna dalili zitakazojitokeza kwa miaka mingi. Uambukizaji unatokea kwenye hatua ya kwanza, ya pili na mara chache mwanzoni mwa hatua ya latent phase.

Hatua Ya kwanza Ya Kaswende โ€“ Primary Syphilis

Kaswende huanza kama mchubuko mmoja (au zaidi ya mmoja) mgumu usio na maumivu unaojulikana kama chancre kwenye sehemu za siri, kwenye mdomo, au kwenye ngoz,i siku 10-90 (wastani wa miezi 3) baada ya maambukizi. Mchubuko huu unaweza kubaki hapo bila kuleta usumbufu kwa kipindi kirefu na hata maiaka mingi. Mchubuko huu wa mviringo hutokea kwenye eneo la maambuikizi. Hata bila ya tiba yo yote, mchubuko huu unaweza ukapona wenyewe bila kuacha kovu katika wiki sita.

Hatua Ya Pili Ya Kaswende โ€“ Secondary Syphilis

Hatua ya pili inaweza ikadumu kwa mwezi mmoja hadi miezi sita ikianza kama wiki sita hadi miezi sita baada ya maambukizi. Dalili Katika hatua ya pili, vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo. Vijipele hivi huwa vya mviringo vyenye rangi nyekundu au vyenye wekundu wa kahawia. Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye sehemu za midomo na mkundu. Vile kutatokea maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa mwili. Latent Syphilis Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa, ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.

Hatua Ya Tatu Ya Kaswende โ€“ Tertiary syphilis

Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya hatua ya tatu โ€“ tertiary syphilis. Hatua hii inatokea miaka 10 hadi 30 baada ya dalili za mwanzo za kaswende. Dalili Dalili za kaswende za hatua hii ni pamoja na kushindwa kumudu matumizi ya viungo vya mwili, ganzi, upofu, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, madhara kwenye moyo na mishipa ya damu, madhara kwenye ini, mifupa na maungio ya mifupa. Kifo huweza kutokea kutokana na uharibifu wa viungo vya mwili.

Matibabu ya ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende unatibika. Kuwahi kumpa tiba mgonjwa wa kaswende ni muhimu kwani kuchelewa kunaweza kumletea madhara makubwa ya mwili au kifo. Kama ugonjwa haujazidi mwaka mmoja, mara nyingi dozi moja ya ya penicillin hutosha. Kaswende iliyoendelea kwenye hatua nyingine, dozi nyingine zitahitajika.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak... Read More

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza... Read More

Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubong... Read More
Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu ... Read More

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sa... Read More

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, โ€˜Potassiumโ€™, โ€˜Magnesiumโ€™ na virutubis... Read More

Faida za kula karanga mbichi

Faida za kula karanga mbichi

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuz... Read More

Jinsi ya Kujitibu kwa njia ya matunda

Jinsi ya Kujitibu kwa njia ya matunda

Yafuatayo ni magonjwa na njia za kujitibu kwa kutumia matunda

KUTUBU KIUNGULIA

Aliy... Read More

Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo ... Read More

Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu

Hatua za kufuata

  1. Chukua Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi i... Read More
Faida za kufanya Masaji kiafya

Faida za kufanya Masaji kiafya

Masaji uongeza kinga ya mwili

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambuki... Read More

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia Binzari, maziwa na asali

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia Binzari, maziwa na asali

Unahitaji vitu vifuatavyo:

a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Baku... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About