Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili.
Ili kuepukana na ugonjwa wa saratani au kupunguza uwezekano wa kupata saratani ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
1. Kula zaidi vyakula vya mimea na nafaka zisizokobolewa
Matokeo ya tafiti yanaonesha kuwa vyakula hivi vinapunguza uwezekano wa kupata saratani, Hakikisha unakula mboga mboga za kijani na rangi nyingine kama njano,zambara. Kula nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona, mchele wa brauni,unga wa ngano usiokobolewa,mtama na ulezi.
2. Kuwa na Uzito Uliosahihi
Uzito mkubwa uliopitiliza ni hatari na husababisha saratani. Hakikisha uwiano wa urefu na uzito wako (BMI- Body -to-Mass Index) ni sahihi ambayo ni 18 -25 kwa mtu mzima na mwenye afya nzuri unashauriwa kuwa na uwiano wa 21-23.
Punguza vyakula vinavyonenepesha mwili kama vyenye mafuta na sukari kwa wingi. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama chipsi na vitumbua mfano ni hatari kwa afya yako.Vyakula vyenye sukari ni kama soda,chokoleti,keki,barafu na iskrimu na juisi bandia.
3. Fanya mazoezi ya mwili
Fanya mazozi ya mwili kila siku. Dakika 15-30 tu zinatosha kufanya mazoezi kwa afya njema. Ukikosa muda fanya anagalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30.
Kukimbia(jogging) ni njia rahisi ya kufanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima. Ukiweza jiunge katika timu ya mpira au klabu za mazoezi ya ndani.
Tembea kwa miguu pale inapobidi. Rafiki yangu mmoja ambaye ana gari ameweka ratiba ya kutotumia gari wakati wa mwisho wa juma. Anapanda dalala na kutembea kwa sehemu kubwa. Unaweza ukafanya hivyo pia.
4. Punguza au Acha kula Nyama nyekundu.
Ukiachia mbali saratani, nyama nyekundu imetambulika kusababisha madhara mengi na makubwa kwa binadamu.
Amua sasa kuachana nayo. Hamia katika samaki na kuku kwa kuanzia na baadae huenda ukaachana na hizo nyingine pia.
Nyama ya nguruwe maarufu kam Kitimoto ni nyama nyekundu na ni hatari kwa afya yako . Heri wale ambao hata dini zao zilikataza nyama hii ya Nguruwe kwani wameepuka hatari.
5. Epukana na Nyama za kusindikwa.
Nyama za makopo na soseji zinasababisha saratani kutokana na kemikali za kutunzia zisioze na pia huwekwa chumvi nyingi sana ambayo ni hatari kwa afya.
6. Punguza Matumizi ya Chumvi
Chumvi ya kupita kiasi inaongeza uwezekano wa kupata saratani hivyo ni hatari. Tumia chumvi kwa kiasi kidogo kwa afya njema. Binadamu anahitaji gramu 5 tu kwa siku sawa na kijoko kidogo cha chai.
Usiongeze chumvi wakati wa kula,chumvi isiyoyeyuka nia hatari zaidi.
7. Acha kula Vyakula vyenye Ukungu
Acha kula nafaka na kundekunde zilizootesha ukungu hasa kwa kutohifadhiwa vyema. Vyakula hivi vinatoa sumu ya aflatoxin
8. Usivute Sigara
Uvutaji wa sigara ni hatari na huenda ukakusababishia saratani ya koo,kinywa na mapafu. Acha kuvuta sigara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani. Fikiria kidogo,kwanini ufe kwa sababu ya moshi tu?.
9. Punguza au Acha Pombe Kabisa
Ukiacha pombe utapunguza uwezekano wa kupata saratani na hivyo kuwa salama zaidi.
Achana na pombe, kuna madhara mengi sana ya kunywa pombe ukiachia ya saratani.
Badilisha Mtindo wa Maisha na Uwe Salama na Saratani
Namna ya kuishi kunachangia kwa kiasi kikubwa kupata saratani au la. Chagua mtindo ulio bora na salama kama ilivyoshauriwa katika mada hii juu ya kuepukana na ugonjwa wa saratani.
Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na kupanga ni kuchagua. Panga kuishi mtindo wa maisha ulio bora na salama chagua kuishi bila saratani.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza...
Read More
Ugonjwa wa Shinikizo la chini la damu ambao hujulikana kama hypotension kwa Kiingereza ni hali am...
Read More
Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanau...
Read More
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw...
Read More
Ili uweze kuwa na siku nzuri basi unashauriwa kuanza siku yako kwa kutumia mchanganyiko wa maji y...
Read More
Mfumo huu wa moyo una kazi zifuatazo:-
๐kupampu damu Mwilini pia kusafirisha gas, taka n...
Read More
Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids....
Read More
Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemengโen...
Read More
Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.
Chemsha maji k...
Read More
Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vya...
Read More
Vifaa vya kieletroniki
Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa ...
Read More
Kitunguu swaumu hujulikana kama kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!