Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:- Uvutaji sigara
- Unene na uzito kupita kiasi
- Unywaji wa pombe
- Upungufu wa madini ya potassium
- Upungufu wa vitamin D
- Umri mkubwa
- Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
- Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Uanishaji wa shinikizo la damu
Presha ya kawaida <120 <80 Presha inayoelekea kupanda 120-139ย 80-89 Presha hatua ya 1ย 140-159ย 90-99 Presha hatua ya 2ย 160-179ย 100-109 Presha hatua ya 3 โฅ180 โฅ110 Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti. Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma. Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes). Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.Dalili zitakazokutokea unapokuwa na ugonjwa huu ni pamoja na;
- Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
- Kuchanganyikiwa,
- Kizunguzungu,
- Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
- Kutoweza kuona vizuri au
- Matukio ya kuzirai.
- Uchovu/kujisikia kuchokachoka
- Mapigo ya moyo kwenda haraka
- Kutokuweza kuona vizuri
- Damu kutoka puani
- Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.
Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:
Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;- Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
- Shambulio la moyo (heart attack)
- Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
- Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
- Kiharusi
- Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
- Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).