Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida za kutembea kwa miguu.
- Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
- Huimarisha mifupa.
- Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
- Husaidia kupunguza uzito.
- Huzuia saratani ya utumbo mpana.
- Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
- Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
- Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito β BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
- Hukabili shinikizo la damu.
- Huondoa msongo wa mawazo.
- Huongeza utayari.
- Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
- Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
- Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
- Huimarisha misuli.
- Husaidia mmengβenyo wa chakula kwenda vizuri.
- Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
- Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
- Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
- Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
- Hukuweka katika hali nzuri (mood).
- Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
- Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
- Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
- Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.