Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu.

Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia waduduโ€”viwatilifu.

Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu โ€” viwatilifu.

1. Husababisha saratani.

Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu.

Hatari hii hutokea zaidi pale ambapo mtu anakula vyakula vilivyoathiriwa na sumu za dawa za kuulia wadudu.

2. Huvuruga mfumo wa homoni.

Mwili wa binadamu huzalisha homoni mbalimbali zinazowezesha viungo mbalimbali kufanya kazi vyema.

Dawa za kuulia wadudu zinapoingia mwilini huathiri mfumo wa homoni wa binadamu na kuufanya usifanye kazi vyema.

3. Huathiri mfumo wa uzazi.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa matatizo ya uzazi kati ya wanaume na wanawake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinapoingia mwilini kupitia matunda au mbogamboga huharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba au utasa.

4. Huharibu ubongo.

Madawa ya kuulia wadudu โ€” viwatilifu huathiri pia mfumo wa ubongo hasa kwa watu wanaoyapulizia au kukaa nayo karibu kwa muda mrefu.

Maradhi kama vile Mild Cognitive Dysfunction (MCD) ambayo humfanya mtu ashindwe kutambua vyema maneno, rangi au namba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

5. Huathiri mama mjamzito na mtoto

Mama mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari nyingi sana wakati wa ujauzito ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.

Matumizi ya viwatilifu ndani ya nyumba au karibu na makazi kwa lengo la kuua wadudu kama vile mbu, chawa, kunguni, au utitiri kunaweza kumwathiri mama mjamzito na mtoto kwa kiasi kikubwa.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa bila viungo vyote, kuzaliwa kabla ya wakati au hata kifo.

6. Huharibu viungo muhimu vya mwili

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ulimwenguni zikieleza kuwa dawa za kuulia wadudu huharibu viungo muhimu vya mwili kama vile figo na ini.

Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.

7. Huathiri mfumo wa upumuaji

Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.

Hivyo ili kujikinga na athari hii inashauriwa kuvaa vifaa bora vya kuzuia kuvuta sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu.

8. Huathiri ngozi

Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.

Ikumbukwe kuwa sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu zinaweza kuingia mwilini kirahisi kupitia ngozi na kusababisha athari nyingi za kiafya.

Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu โ€” viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.

Ikumbukwe kuwa vifo vingi na matatizo mbalimbali ya kiafya hutokana na mwili wa binadamu kukutana na sumu mbalimbali, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Madhara ya kumlaza mtoto kifudifudi, kumlaza kwa tumbo

Madhara ya kumlaza mtoto kifudifudi, kumlaza kwa tumbo

Unafahamu nini kuhusu suala la kumlaza mwanao? Maana Mapokeo tuliyo yapokea enzi na enzi ni kuwa ... Read More

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu ... Read More

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chem... Read More
Faida za kufanya Masaji kiafya

Faida za kufanya Masaji kiafya

Masaji uongeza kinga ya mwili

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambuki... Read More

Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 โ€“ 70 ya wanaume hupotez... Read More

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa mais... Read More
Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali

Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya as... Read More

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinaz... Read More
Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Chunusi ni nini?