Dalili za kifua kikuu.
- Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
- Maumivu ya kifua
- Homa za usiku
- Kutoka jasho kwa wingi usiku
- Kupungua uzito
- Kukohoa damu
- Kukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu
Athari za kifua kikuu.
- Ugonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili.
- Watu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema.
- Watu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi.
- Wagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea.
- Matibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa.
Kinga za ugonjwa wa kifua kikuu.
Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa.Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;
- Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)
- Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi
- Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara
- Kula vyakula vyenye lishe bora
- Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.