Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/katoliki/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kufurahisha na Watoto: Kujenga Kumbukumbu za Kucheka

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kufurahisha na Watoto: Kujenga Kumbukumbu za Kucheka

Leo hii, nataka kuzungumzia jinsi ya kuwa na mazungumzo ya kufurahisha na watoto. Ni muhimu sana ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Kuwajibika na kufanya maamuzi muhimu ya kifamilia ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kudumu. Hapa kuna ... Read More
Jinsi ya Kuweka Mipaka ya Familia: Kuimarisha Uhusiano na Kuheshimu Uhuru wa Kila Mtu

Jinsi ya Kuweka Mipaka ya Familia: Kuimarisha Uhusiano na Kuheshimu Uhuru wa Kila Mtu

  1. Kuweka mipaka ya familia ni jambo muhimu sana katika kuboresha uhusiano kati ya wanafam... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kuwa na Marafiki Pamoja

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kuwa na Marafiki Pamoja

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Nafasi ya Kuwa na Marafiki Pamoja

<... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na kuunga mkono ndoto za kila mmoja

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mazingira ya upendo na kuunga mkono ndoto za kila mmoja

Kuwa na mpenzi ambaye mnashirikiana ndoto na kujenga maisha pamoja ni mojawapo ya vitu vizuri zai... Read More

Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Ukuaji na Maendeleo katika Familia

Jinsi ya Kujenga Mazingira ya Ukuaji na Maendeleo katika Familia

Familia ni kitovu cha maendeleo yoyote yale katika jamii yetu. Hivyo basi, ni muhimu sana kuwa na... Read More

Kufurahisha Katika Njia Mpya: Kujaribu Mazoea Mapya ya Kufanya Mapenzi

Kufurahisha Katika Njia Mpya: Kujaribu Mazoea Mapya ya Kufanya Mapenzi

Kufurahisha Katika Njia Mpya: Kujaribu Mazoea Mapya ya Kufanya Mapenzi

  1. Mapenzi ni se... Read More
Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada wakati wa Shida na Msukumo wa mke wako

Kuwa msaada wakati wa shida na msukumo kwa mke wako ni jambo muhimu katika kuimarisha uhusiano na ku... Read More
Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha yetu, hasa yale ya kimapenzi. Ndio maana ni muhimu s... Read More

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako

Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako ni muhimu kwa ustawi wa uhusiano wenu na kul... Read More
Kufanya Mapenzi na Kuzeeka: Kufurahia Intimiteti katika Hatua Zote za Maisha

Kufanya Mapenzi na Kuzeeka: Kufurahia Intimiteti katika Hatua Zote za Maisha

Kufanya Mapenzi na Kuzeeka: Kufurahia Intimiteti katika Hatua Zote za Maisha

Kuna wakati m... Read More

Jinsi ya Kujenga furaha na uchangamfu katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga furaha na uchangamfu katika uhusiano na mpenzi wako

Kujenga furaha na uchangamfu katika uhusiano wako na mpenzi wako ni jambo muhimu katika kudumisha uh... Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About