Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
FROM FR TITUS AMIGU
Siku moja, miaka kama 14 hivi iliyopita, nilimzingua mchungaji wa kikanisa fulani. Alinijia mbio na kuniambia, "Ati… Kadinali wenu amesema kuwa pombe sio dhambi! Kwanini usihame huko? Angalia sasa, hata kiongozi wenu wa juu wa Kanisa amekosea kwa kusema pombe sio dhambi."
Basi mimi nikamjibu huyo mzee kama ifuatavyo;
Je kisu ni dhambi? Mzee akajibu, "hapana!" Je sumu ya panya? Mzee akajibu tena, "hapana". Nikampa changamoto hii; Je, kama mtu akimdunga mwenzake kisu na kumuua, hapo dhambi ni kisu au kuua? Au mtu afanyaye kujiua kwa kumeza sumu ya panya, je basi ndio tuseme kuwa sumu ya panya ni dhambi? Mzee akajibu, hapana.
Nikamkumbusha maneno ya Yesu kuwa kitu kimuingiacho mtu hakiwezi kumtia unajisi.
Nikamwambia, "Kanisa lako ni kanisa la walevi." Mzee akatumbua macho, "… hee… kijana wewe?…" Nikamweleza;
Wengi kama si wote, wa wafuasi katika kanisa lenu ni walevi. Wanatamani kunywa na kulewa, lakini wewe kama mchungaji umewazuia kwa sheria, tena sheria kali yenye vitisho na kuwatia hofu. Umeweka mikono yako machoni pao na kuwaambia kuna shimo mbele, hivyo umewafanya vipofu zaidi. Kila mwanamume amtazamaye mwanamke kwa tamaa amekwisha kuzini naye moyoni , na vivyo hivyo, kila atamaniye ulevi amekwisha kulewa moyoni ; hata kama asipoonja pombe, ni mlevi tu.
Nikazidi kumweleza kuwa mimi niliimarishwa (Kipaimara) kwa kuwekewa mikono na Askofu, nikaombewa ujazo wa Roho Mtakatifu. Kunywa ama kutokunywa nafanya si kwa amri, bali kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Sheria ya usionje, usiguse hainihusu, maana mimi ni mtu huru katika Roho. Kwa hiyo siwezi kujiunga na kanisa la walevi, ambao badala ya kumtii Mungu, wanaitii hofu iliyopandwa ndani yao.
Yule mzee akasema, hapo umenijibu vema kijana, lakini mbona ninyi Wakatoliki mnawaomba wafu, kama Bikira Maria? Nikamjibu,;
Sisi Wakatoliki ni Kanisa lililo katika ushirika wa Watakatifu. Yesu aliwaambia Masadukayo kuwa Bwana ni Mungu wa walio hai, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Ndio maana pale mlimani Yesu alipogeuka sura aliongea na Musa na Eliya walio hai. Katika kikanisa chenu hakuna imani ya kuweza kuongea na Yesu ili muingie katika utukufu wake, na awawezeshe kuongea na Musa na Eliya, Bikira Maria au watakatifu wengine walio hai katika Bwana. Mkifa, mnakufa kama mbwa, na mnakufa kweli kweli. Basi siko tayari kujiunga na kanisa la wafu, tena wasio na imani ya kuona mambo ya rohoni. Japo mnajiita kanisa la kiroho, mambo ya rohoni hamyajui, maana ninyi ni kanisa la wafu.
Yule mzee akazua ghafla safari ya kwenda kunywa chai aliyodai ameitwa na mjukuu wake akanywe, naye faster akasepa.
Je, waijua misingi ya imani yako? Je, unaongozwa na Roho Mtakatifu au na sheria za kidini?
Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho.
AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Robert Ndunguru Guest Apr 9, 2024
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
πŸ‘₯ Chris Okello Guest Apr 1, 2024
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
πŸ‘₯ Violet Mumo Guest Mar 26, 2024
Endelea kuwa na imani!
πŸ‘₯ Margaret Anyango Guest Feb 18, 2024
Mungu ni mwema, wakati wote!
πŸ‘₯ Margaret Mahiga Guest Feb 15, 2023
Rehema zake hudumu milele
πŸ‘₯ Esther Nyambura Guest Dec 8, 2022
Kwa Mungu, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Francis Mrope Guest Nov 22, 2022
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
πŸ‘₯ Elizabeth Mrope Guest Sep 27, 2022
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
πŸ‘₯ Christopher Oloo Guest Sep 15, 2022
Wakati wa Mungu ni kamilifu
πŸ‘₯ George Wanjala Guest Sep 15, 2022
Nakuombea πŸ™
πŸ‘₯ Wilson Ombati Guest Jun 11, 2022
Rehema hushinda hukumu
πŸ‘₯ Victor Kimario Guest Apr 28, 2022
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
πŸ‘₯ Dorothy Mwakalindile Guest Apr 24, 2022
Mwamini Bwana; anajua njia
πŸ‘₯ Lydia Mahiga Guest Feb 12, 2022
Sifa kwa Bwana!
πŸ‘₯ Moses Kipkemboi Guest Oct 26, 2021
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
πŸ‘₯ Lucy Wangui Guest Sep 30, 2021
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
πŸ‘₯ Wilson Ombati Guest Apr 9, 2021
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
πŸ‘₯ Catherine Naliaka Guest Jan 3, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
πŸ‘₯ Henry Sokoine Guest Nov 19, 2020
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
πŸ‘₯ Kenneth Murithi Guest Oct 23, 2020
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
πŸ‘₯ Emily Chepngeno Guest Jul 18, 2020
Imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Alex Nyamweya Guest Mar 28, 2020
Mungu akubariki!
πŸ‘₯ Emily Chepngeno Guest Mar 23, 2020
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
πŸ‘₯ Richard Mulwa Guest Jan 8, 2020
Dumu katika Bwana.
πŸ‘₯ Michael Onyango Guest Dec 12, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
πŸ‘₯ Irene Akoth Guest Nov 1, 2019
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
πŸ‘₯ Nancy Komba Guest Oct 4, 2019
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
πŸ‘₯ Paul Kamau Guest Sep 16, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
πŸ‘₯ Catherine Naliaka Guest Aug 23, 2019
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
πŸ‘₯ Frank Macha Guest Aug 5, 2019
Katika imani, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Moses Kipkemboi Guest Apr 24, 2019
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
πŸ‘₯ David Kawawa Guest Mar 16, 2019
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
πŸ‘₯ Lydia Mzindakaya Guest Dec 19, 2018
Tembea kwa imani, si kwa kuona
πŸ‘₯ Peter Mbise Guest Dec 5, 2018
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
πŸ‘₯ James Mduma Guest Aug 12, 2018
Mwamini katika mpango wake.
πŸ‘₯ Vincent Mwangangi Guest Apr 12, 2018
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
πŸ‘₯ George Wanjala Guest Mar 2, 2018
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
πŸ‘₯ Rose Lowassa Guest Nov 29, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Isaac Kiptoo Guest Aug 30, 2017
Tumaini ni nanga ya roho
πŸ‘₯ Andrew Odhiambo Guest Jul 1, 2017
Neema na amani iwe nawe.
πŸ‘₯ Charles Wafula Guest Jun 13, 2017
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
πŸ‘₯ Charles Wafula Guest Mar 6, 2017
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
πŸ‘₯ Brian Karanja Guest Feb 11, 2017
Nguvu hutoka kwa Bwana
πŸ‘₯ Peter Mugendi Guest Nov 24, 2016
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
πŸ‘₯ Samson Mahiga Guest Nov 10, 2016
Neema ya Mungu inatosha kwako
πŸ‘₯ George Wanjala Guest Jul 11, 2016
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
πŸ‘₯ John Lissu Guest Jun 30, 2016
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
πŸ‘₯ Henry Sokoine Guest Oct 28, 2015
Baraka kwako na familia yako.
πŸ‘₯ Stephen Kikwete Guest Sep 5, 2015
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Anna Sumari Guest Aug 19, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About