Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ

MASOMO YA MISA, MACHI 17, 2022: ALHAMISI, JUMA LA 2 LA KWARESIMA

โ€ข
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

SOMO 1

Yer. 17:5-10

Bwana asema hivi: Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo na ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda. Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. Neno la Bwanaโ€ฆ Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 1:1-4, 6 (K) 40:4

(K) Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake. Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K) Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. (K) Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kw akuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. (K)

SHANGILIO

Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako.

INJILI

Lk. 16:19-31

Yesu aliwaambia Mafarisayo: Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwaninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao piawakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu. Neno la Bwanaโ€ฆ Sifa kwako Ee Kristo.
AckySHINE Solutions
โœจ Join AckySHINE for more features! โœจ

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
๐Ÿ‘ฅ Andrew Mahiga Guest Dec 22, 2023
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
๐Ÿ‘ฅ Peter Tibaijuka Guest Nov 27, 2023
Baraka kwako na familia yako.
๐Ÿ‘ฅ Lucy Kimotho Guest Oct 7, 2023
Mwamini Bwana; anajua njia
๐Ÿ‘ฅ Grace Majaliwa Guest Oct 5, 2023
Nguvu hutoka kwa Bwana
๐Ÿ‘ฅ John Malisa Guest Jun 18, 2023
Mungu akubariki!
๐Ÿ‘ฅ Francis Mrope Guest Nov 30, 2022
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
๐Ÿ‘ฅ Thomas Mwakalindile Guest Sep 26, 2022
Neema na amani iwe nawe.
๐Ÿ‘ฅ Ruth Mtangi Guest Aug 8, 2022
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
๐Ÿ‘ฅ Rose Mwinuka Guest Jul 30, 2022
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
๐Ÿ‘ฅ Elizabeth Malima Guest May 1, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
๐Ÿ‘ฅ Hellen Nduta Guest Feb 26, 2022
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
๐Ÿ‘ฅ Andrew Mchome Guest Sep 21, 2021
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
๐Ÿ‘ฅ Joy Wacera Guest Sep 17, 2021
Wakati wa Mungu ni kamilifu
๐Ÿ‘ฅ Ruth Kibona Guest Sep 6, 2021
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
๐Ÿ‘ฅ Richard Mulwa Guest Sep 4, 2021
Katika imani, yote yanawezekana
๐Ÿ‘ฅ Janet Mwikali Guest Jul 20, 2021
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
๐Ÿ‘ฅ Moses Mwita Guest Jul 13, 2021
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
๐Ÿ‘ฅ Andrew Mchome Guest Apr 23, 2021
Rehema zake hudumu milele
๐Ÿ‘ฅ Edwin Ndambuki Guest Mar 17, 2021
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
๐Ÿ‘ฅ Josephine Nekesa Guest Mar 4, 2021
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
๐Ÿ‘ฅ Janet Mwikali Guest Jan 23, 2021
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
๐Ÿ‘ฅ Janet Mwikali Guest Nov 29, 2020
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
๐Ÿ‘ฅ Nicholas Wanjohi Guest Jul 18, 2020
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
๐Ÿ‘ฅ Elizabeth Mtei Guest Jun 20, 2020
Rehema hushinda hukumu
๐Ÿ‘ฅ Samuel Were Guest Jun 13, 2020
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
๐Ÿ‘ฅ Joyce Mussa Guest Dec 24, 2019
Sifa kwa Bwana!
๐Ÿ‘ฅ Stephen Amollo Guest Apr 17, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
๐Ÿ‘ฅ James Kawawa Guest Apr 16, 2019
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
๐Ÿ‘ฅ Grace Mushi Guest Feb 17, 2019
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
๐Ÿ‘ฅ James Malima Guest Dec 18, 2018
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
๐Ÿ‘ฅ Mercy Atieno Guest Nov 25, 2018
Endelea kuwa na imani!
๐Ÿ‘ฅ Simon Kiprono Guest Jan 22, 2018
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
๐Ÿ‘ฅ Faith Kariuki Guest Nov 29, 2017
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
๐Ÿ‘ฅ Charles Mchome Guest Sep 11, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
๐Ÿ‘ฅ Joseph Kawawa Guest Jun 22, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
๐Ÿ‘ฅ Paul Kamau Guest Jun 13, 2017
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
๐Ÿ‘ฅ Grace Minja Guest May 10, 2017
Tembea kwa imani, si kwa kuona
๐Ÿ‘ฅ Joyce Nkya Guest Mar 19, 2017
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
๐Ÿ‘ฅ Victor Malima Guest Jan 3, 2017
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
๐Ÿ‘ฅ Victor Sokoine Guest Oct 24, 2016
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
๐Ÿ‘ฅ Dorothy Nkya Guest Oct 22, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
๐Ÿ‘ฅ Catherine Mkumbo Guest Sep 18, 2016
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
๐Ÿ‘ฅ Sarah Karani Guest Aug 15, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
๐Ÿ‘ฅ Peter Mwambui Guest Aug 4, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
๐Ÿ‘ฅ Alice Mrema Guest Jul 22, 2016
Kwa Mungu, yote yanawezekana
๐Ÿ‘ฅ Stephen Amollo Guest Jun 18, 2016
Mungu ni mwema, wakati wote!
๐Ÿ‘ฅ Anna Sumari Guest Apr 3, 2016
Mwamini katika mpango wake.
๐Ÿ‘ฅ Anna Mahiga Guest Jan 17, 2016
Neema ya Mungu inatosha kwako
๐Ÿ‘ฅ Lydia Wanyama Guest Dec 27, 2015
Dumu katika Bwana.
๐Ÿ‘ฅ Diana Mallya Guest Nov 27, 2015
Nakuombea ๐Ÿ™

๐Ÿ”— Related Posts

๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About