Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;
Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:
- Kukojoa mara chache sana
- Mdomo na ulimi kukauka
- Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
- Mtoto kutokuwa mchangamfu
- Macho, tumbo au mashavu kubonyea
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki. Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.
Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:- Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
- Kuumwa na kichwa.
- Mwili kukosa nguvu.
- Kichefuchefu na kutapika.
- Kukaukwa na mdomo.