Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
ยท Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
ยท Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
ยท Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
ยท Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
ยท Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
ยท kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
ยท Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
ยท Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
ยท Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua...
Read More
Ni kazi ngumu kidogo kuacha uvutaji wa sigara. Uvutaji ni tishio kwa maisha yetu. Yawezekana hufa...
Read More
Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingere...
Read More
Ugonjwa wa Shinikizo la chini la damu ambao hujulikana kama hypotension kwa Kiingereza ni hali am...
Read More
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupi...
Read More
Korosho zina faida hizi zifuatazo;
1. Zinakinga Maradhi ya Saratani Haswa kwenye matumbo ma...
Read More
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho n...
Read More
Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Kupooza ubongo kitaalamu ni Cerebral plasy (CP), ni hali ya kupooz...
Read More
Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka?
Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi...
Read More
Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini i...
Read More
Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanau...
Read More
Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanao...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!